China yatoa Sh345 milioni kusaidia fani ya uvuvi Veta Chato

Wazifri wa Mambo ya Nje wa China Mhe. Wang Yi akiwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia wa Tanzania Profesa Joyce Ndalichako, Wazairi wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi na Mwenyekiti wa Bodi ya VETA  Bw. Peter Maduki

Muktasari:

Ziara ya Waziri wa China yaja na neema nchini atoa msaada wa dola za Marekani Sh 1,50000 kwa ajili ya kuendeleza uvuvi katika chuo cha kisasa cha ufundi stadi cha Chato.

Dar es Salaam.  Serikali ya China imekabidhi msaada wa dola za Marekani 1,50000 kwa ajili ya kuendeleza fani ya uvuvi katika chuo cha kisasa cha Ufundis Stadi (Veta) kilichopo Chato mkoani Geita.
 
Msaada huo ulitolewa leo Ahamisi Januari 7, 2020 na Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi muda mfupi baada ya kuzindua chuo hicho akishirikiana na Waziri wa Elimu, Joyce Ndalichako.
 
Yi ambaye yupo katika ziara kwenye bara la Afrika atakuwa Tanzania kwa siku mbili amewasili leo na katika uwanja wa Ndege wa Chato-Geita na kupokelewa na mwenyeji wake, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Profesa Palamagamba Kabudi.
 
Akiwa katika chuo hicho cha Veta, YI amesema “China itaendelea kuisadia vyuo vya ufundi stadi na kwa niaba ya Serikali ya China natoa msaada wa fedha za China Sh 1milioni,”
 
“Rais wa Tanzania amejenga vyuo vingi vya ufundi katika mikoa mbalimbali kikiwamo hiki cha Chato. China pia inajisikia faraja kujenga vyuo vya ufundi kikiwamo cha Kagera ambacho kikikamirika kitakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 1,000 pamoja na programu zote,” amesema Yi huku akishangiliwa.
 
Yi amewahikikisha Watanzania kuwa balozi wa nchi hiyo ataendelea kuwepo Tanzania na kwamba endapo chuo cha Veta kitahitaji mahitaji yoyote kimwambie huku akisema Tanzania ili isonge na kupata mafanikio inahitaji vijana wengi wenye ujuzi.
 
“China na Tanzania ni marafiki wakubwa duniani, najisikia furaha kuzindua jengo hili,” amesema Yi ambaye pia ni mwanadiplomasia na mjumbe wa kamati ya kitaifa ya China.