Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chongolo atoa maagizo kwa DC mpya Mbozi

Mkuu mpya wa Wilaya ya Mbozi, Hamad Mbega akila kiapo leo Januari 29,2025 katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa Nselewa wilayani Mbozi. Picha na Denis Sinkonde

Muktasari:

  • Chongolo amemtaka Mbega kuchukua hatua madhubuti dhidi ya uhalifu, hususan vitendo vya ulawiti na ubakaji, pamoja na kuhakikisha mazingira yanahifadhiwa kwa maendeleo endelevu ya wilaya hiyo.

Songwe. Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo, amemuagiza mkuu mpya wa wilaya ya Mbozi, Hamad Mbega kusimamia ipasavyo masuala ya mimba za utotoni, udumavu, na mdondoko wa ufaulu ili kuondoa changamoto inayolikabili kundi hilo, wakiwepo watoto.

Mbega, ameapishwa leo Jumatano, Januari 29, 2025, katika hafla fupi iliyofanyika katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Songwe, zilizopo eneo la Selewa.

Mkuu huyo wa wilaya, aliteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan Januari 24, 2025, kuchukua nafasi ya Ester Mahawe, aliyefariki dunia hivi karibuni.

Akizungumza baada ya kumuapisha mkuu huyo wa wilaya, Chongolo, amemtaka Mbega kutumia ujuzi wake kuhakikisha wilaya hiyo inapiga hatua za maendeleo.

Ametumia fursa hiyo kumpatia majukumu mahususi ya kuanzia ambayo ni kudumisha amani na utulivu, huku akimtaka kutilia mkazo masuala muhimu kama mimba za utotoni, mdondoko wa wanafunzi shuleni, pamoja na suala la udumavu, kwani licha ya wilaya hiyo kuwa miongoni mwa wazalishaji wa chakula, bado viwango vya udumavu viko juu.

Aidha, Chongolo amemtaka Mbega kuchukua hatua madhubuti dhidi ya uhalifu, hususan vitendo vya ulawiti na ubakaji, pamoja na kuhakikisha mazingira yanahifadhiwa kwa maendeleo endelevu ya wilaya hiyo.

Akitoa neno la shukrani baada ya kuapishwa, Mbega amemshukuru Rais Samia kwa kumuamini na kumpatia nafasi ya kuongoza wilaya hiyo.

Mbega ameahidi kufanya kazi kwa bidii na kushirikiana na viongozi pamoja na wananchi kuhakikisha maendeleo yanapatikana katika Wilaya ya Mbozi.