Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chuo cha Kilimo Butiama ‘chatwishwa’ zigo ukosefu wa ajira

Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ushauri Kitaaluma na Kitaalamu ya Chuo Kikuu cha Mwalimu Julius Nyerere cha Kilimo na Teknolojia (MJNUAT) wakiwa kwenye hafla ya uzinduzi wa kamati hiyo iliyofanyika mjini Musoma Mei 3, 2023. Picha na Beldina Nyakeke

Muktasari:

Kamati ya Ushauri Kitaalamu na Kitaaluma ya Chuo Kikuu cha Mwalimu Julius Nyerere cha Kilimo na Teknolojia (MJNUAT) kimetakiwa kuweka mikakati itakayowezesha chuo hicho kutoa wahitimu wenye ujuzi na maarifa yatakayochochea maendeleo kwa kupunguza tatizo la ajira nchini.

Musoma. Kamati ya Ushauri Kitaalamu na Kitaaluma ya Chuo Kikuu cha Mwalimu Julius Nyerere cha Kilimo na Teknolojia (MJNUAT) kimetakiwa kuweka mikakati itakayowezesha chuo hicho kutoa wahitimu wenye ujuzi na maarifa yatakayochochea maendeleo kwa kupunguza tatizo la ajira nchini.

Akizungumza wakati wa hafla ya kuzindua kamati hiyo iliyofanyika mjini Musoma Mei 3, 2023, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Suleiman Mzee amesema mtaala wa chuo hicho unatakiwa kujikita kwenye mbinu za kuwezesha wahitimu kutambua na kutumia fursa za kiuchumi zilizopo katika maeneo yao kujiajiri na kutengeneza ajira kwa wengine

"Kwa mfano, Mkoa wa Mara una fursa nyingi katika sekta za madini, kilimo, utalii na uvuvi; lakini bado hazijatumika vema, sababu kuu ikiwa ni kukosekana kwa utaalam na wataalamu. Ni matarajio yetu kuwa uwepo wa chuo hiki utatatua changamoto hiyo,’’ amesema Mzee

Mkuu huyo wa mkoa ametaja eneo linguine muhimu la kutiliwa maanani katika maandalizi na utekelezaji wa shughuli za chuo hicho kuwa utafiti wa sababu na suluhisho wa changamoto zilizopo ndani ya jamii kwa maendeleo endelevu ya Taifa.

Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo cha MJNUAT, Profesa Lesakit Mellau amesema moja ya malengo ya chuo ni kuzalisha wahitimu wenye ujuzi na maarifa yatakayowawezesha siyo tu kujiajiri, bali pia kutengeneza fursa za ajira kwa wengine.

"Tunataka wahitimu wetu siyo tu wakidhi vigezo na mahitaji ya soko la ajira ndani na nje ya nchi, bali pia wenye uwezo wa kujiajiri na kutoa fursa za ajira kwa wengine " amesema

Akizungumzia shughuli za kamati iliyozinduliwa yenye wajumbe 22, Profesa Mellau ametaja moja ya majukumu muhimu itakuwa ni kushauri uandaaji wa mitaala na kuboresha mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi na watumishi  wa  chuo.

"Wajumbe wa kamati hii ni wadau kutoka sekta binafsi na ya umma wakiwemo waajiri na wana taaluma ambao tunaamini mchango wao utaleta matokeo chanya kitaaluma kwa chuo chetu" amesema Profesa Mellau

Mratibu wa mradi wa ujenzi wa chuo hicho, Profesa Msafiri Jackson amesema kazi hiyo iko katika hatua ya kumpata mkandarasi mshauri na tayari Serikali imetoa zaidi ya Sh102.3 bilioni kwa ajili ya shughuli mbalimbali za chuo.

“Tunajiandaa kutangaza tenda kwa lengo la kupata wakandarasi wenye uwezo watakaojenga miundombinu ya chuo chetu. Tutatumia kampuni tano tofauti katika shughuli ya ujenzi nia ikiwa siyo tu kukamilisha mradi huu kwa haraka, bali pia kwa ubora kulingana na thamani halisi ya fedha," amesema Profesa Jackson