Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dar, Tanga ziko nyuma uwekaji anuani za makazi

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye akizungumza katika katika uwanja wa ndege jijini Dodoma kabla ya kuanza ziara ya kuzunguka nchi nzima kufanya uhamasishaji wa uwekaji anuani za makazi. Picha na Habel Chidawali

Muktasari:

  • Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye na timu yake leo Jumatatu April 11, 2022 wameanza ziara ya kuzunguka nchi nzima kufanya uhamasishaji wa uwekaji anuani za makazi.

Dodoma. Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye ameitaja mikoa ya Tanga na Dar es Salaam kuwa bado haijafanya vizuri kwenye uwekaji wa anuani za makazi.

Nape ametoa kauli hiyo leo Jumatatu April 11, 2022 akiwa katika uwanja wa ndege jijini Dodoma wakati anaanza safari ya kuzunguka nchi nzima kufanya uhamasishaji wa uwekaji anuani za makazi.

Waziri Nape amesema shughuli hiyo ya uwekaji wa anuani za makazi nchini inatakiwa kuhitimishwa Mei 22, 2022 ingawa kwa sasa imefikia wastani wa asilimia 68 kwa nchi nzima.

Leo Waziri huyo akiwa na timu yake wameanzia ziara hiyo mikoa ya Tanga, Kilimanjaro na Arusha.

Amesema katika baadhi ya maeneo wanalazimika kuongeza nguvu kupeleka wataalamu zaidi.