DC amtupa rumande mfamasia

Muktasari:

Kipole alisema jana kuwa awali alipokea taarifa kutoka kwa raia mwema kuhusu dawa kuhamishwa kutoka bohari kupelekewa kusikojulikana na alipofuatilia aliwakuta watu wakisomba masanduku hayo kwa kutumia usafiri wa pikipiki.

Sengerema. Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Emmanuel Kipole amemweka ndani mfamasia wa halmashauri hiyo akituhumiwa kuhamisha masanduku 10 ya dawa bila maelezo.

Kipole alisema jana kuwa awali alipokea taarifa kutoka kwa raia mwema kuhusu dawa kuhamishwa kutoka bohari kupelekewa kusikojulikana na alipofuatilia aliwakuta watu wakisomba masanduku hayo kwa kutumia usafiri wa pikipiki.

“Mwendesha bodaboda aliyekuwa akiyachukua alitimua mbio na kutokomea baada ya kubaini anafuatiliwa,” alisema Kipole