DC apania kuondoa aibu ya mauaji ya vikongwe
Muktasari:
Alisema kukatwa mapanga kwa vikongwe ni aibu kwa Taifa, hivyo kila mmoja awe mlinzi ili mzee asidhuriwe.
Shinyanga. Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro amesema amedhamiria kuliondolea Taifa aibu ya mauaji ya vikongwe.
Alisema kukatwa mapanga kwa vikongwe ni aibu kwa Taifa, hivyo kila mmoja awe mlinzi ili mzee asidhuriwe.
Aliwataka viongozi, wanasiasa na jamii kulilinda kundi hilo kwa nguvu zote.