Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

DC Chikoka ahimiza amani, upendo uchaguzi mkuu

Baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Musoma wakishiriki kwenye bonanza maalum la kuhamasisha amani, upendo na mshikamno kuelekea uchaguzi mkuu. Picha na Beldina Nyakeke

Muktasari:

  • Bonanza hilo maalum mbali na kuboresha afya lakini pia linalenga kujenga mahusiano mazuri kati ya wananchi, watumishi wa umma na binafsi katika kuelekea uchaguzi mkuu.

Musoma. Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Juma Chikoka amewaongoza wakazi wa Manispaa ya Musoma katika bonanza maalum la michenzo lenye lengo la kuhamsisha amani, upendo, ushirikiano na amani kuelekea uchaguzi mkuu.

Akizungumza katika bonanza hilo leo Jumamosi Juni 28,2025 ,Chikoka amesema amani, ushirikiano,upendo na umoja ni nguzo muhimu katika kufanikisha uchaguzi huo ambao ni muhimu kwa ustawi wa nchi na maendeleo ya wananchi.

"Tukiwa tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu tumeona kuna haja ya wananchi kuwa wamoja na wenye ushirikiano huku tukilinda amani yetu na ili kufanikisha hilo, michezo ni jukwaa ambalo likitumika vema tunaweza kufikia malengo haya,"amesema 

Chikoka amesema bonanza hilo litakuwa endelevu hadi pale uchaguzi mkuu utakapofanyika ambapo amesema litakuwa likifanyika kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi.

Amesema ili uchaguzi uweze kufanikiwa ushiriki wa kila mwana jamii ni jambo la muhimu hivyo kupitia mabonaza hayo mbali na ushirikiano wananchi pia watapata hamasa na kuona umuhimu wa kuwa na umoja.

Baadhi wa washiriki wa bonanza  hilo wamepongeza uongozi wa serikali wilayani Musoma kwa kuja na wazo hilo la kufanya mabonanza ili kuhamaisha ushiriki wa wananachi katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Musoma,  Fahamu Mtulya amesema ushiriki wa wananchi kwenye uchaguzi ni haki ya kikatiba na hivyo kutoa wito kwa kila mmoja mwenye sifa kuhakikisha  anashiriki.

"Kuchagua au kuchaguliwa ni haki ya kikatiba ya kila mtu mwenye sifa,hivyo niwaombe watanzania wenzangu kuhakikisha kila mmoja anashiriki kwa nafasi yake kamwe tusipange kukosa suala hili la muhimu kwa maendeleo na ustawi wa nchi yetu," amesema 

Katibu wa Jumuiya ya Maridhiano ya Amani Wilaya ya Musoma, Yusufu Juma watanzania wanatakiwa kuweka kipaumbele katika amani wakati wakijiandaa kushiriki katika uchaguzi mkuu.

"Tunapaswa kulinda amani yetu kwa wivu mkubwa,kamwe tusikubali uchaguzi uwe chanzo cha kuvunjika kwa amani,nimpongeze mkuu wetu wa wilaya kwa kubuni jambo hili ambalo kwa hakika litatumika kuhamaisha amani miongoni mwetu sisi wana jamii," amesema 

Amesema kila mwanajamii kwa nafasi yake anapaswa  kuhakikisha kuwa anakuwa balozi wa amani nchini kwa maelezo kuwa bila amani hakuna maendeleo.

Ester Galibona amesema mbali na kuhamsisha amani na mshikamno kuelekea uchaguzi mkuu, bonanza hilo pia linasaidia katika kuboresha afya za washiriki.

"Tunajua mazoezi ni afya na hapa kuna michezo ya aina mbalimbali hivyo pamoja na kuwa tunajemlnga mahusiano pia tunaboresha afya zetu niombe tu mabonanza kama haya yawe yanafanyika mara kwa mara," amesema