Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Diaspora waitwa kuwekeza, mfuko uwekezaji dola ukizinduliwa nchini

Mmoja wa wakurugenzi wa iTrust Finance Limited,  profesa Mohamed Warsame akizungumza wakati wa uzinduzi wa mfuko wa uwekezaji wa dola.

Muktasari:

  • Katika uwekezaji huo kiwango cha chini cha uwekezaji  ni Dola 1,000  na kiwango cha chini cha ziada ni dola 100 huku muda wa kuweka bila kutoa ikiwa ni siku 90.

Dar es Salaam. Tanzania imezindua mfuko wa kwanza wa uwekezaji wa sarafu ya Dola (iDollar), ukitajwa kuwa hatua muhimu katika maendeleo ya masoko ya fedha na mitaji nchini.

Mfuko huo ulioanzishwa na iTrust Finance Limited na kusimamiwa na CRDB Bank Plc umezinduliwa leo Julai 10, 2025 jijini Dar es Salaam huku Watanzania waishio nje ya nchi wakihimizwa kuwekeza kutokana na urahisi wake.

"Wawekezaji hawahitaji kubadilisha shilingi za Kitanzania kuwa dola ili kuwekeza, hii itawarahisishia hata Diaspora kuwekeza," amesema Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Nicodemus Mkama.

Mkama amesema kuanzishwa kwa mfuko huo kunaifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi za Afrika zinazotoa huduma hiyo ya uwekezaji.

Amezitaja nchi nyingine ni Kenya, Afrika Kusini, Mauritius na Ghana.

Mkama amesema mfuko huo sasa utawezesha Watanzania kuwekeza katika sarafu za kimataifa kama Dola ya Marekani na Pauni ya Uingereza kupitia jukwaa rasmi, salama na linalotambuliwa kisheria.

"Mfuko huu unatoa fursa hasa kwa Watanzania wanaopokea au kutuma fedha za kigeni, kuhifadhi thamani ya fedha zao kupitia uwekezaji unaosimamiwa kitaalamu bila kukosa thamani ya fedha zao," amesema ofisa huyo.

Amefafanua kwamba kwa Watanzania walioko nyumbani na wale walioko nje ya nchi, mfuko wa iDollar unatoa si tu fursa ya uwekezaji, bali pia njia ya kushiriki na kuchangia katika mabadiliko ya kiuchumi ya nchi.

"Mfuko unawalenga watu binafsi, taasisi, na hasa diaspora wa Kitanzania kwa kuwapatia chombo salama cha uwekezaji wa dola bila kuhitaji kubadilisha fedha," amesema.

Mmoja wa wakurugenzi wa iTrust Finance,  Profesa Mohamed Warsame amesema mfuko huo ni uwekezaji ulio salama, katika hati fungani za muda mfupi hadi wa kati ambao unatoa mapato bora zaidi kulingana na amana za kudumu za benki za dola.

"Mfuko huu ni rahisi katima upatikanaji wa fedha, uwekezaji mseto, pamoja na usalama dhidi ya mabadiliko ya thamani ya Shilingi ya Tanzania, vyote vikiwa chini ya usimamizi wa kitaalamu na udhibiti wa kisheria.

"Umelenga kutoa mapato ya ushindani kwa kuwekeza kwenye dhamana zenye mapato ya kudumu za dola, ikiwa ni pamoja na amana za muda na hati fungani za makampuni binafsi," amesema.

Katika uwekezaji huo, kiwango cha chini cha uwekezaji  ni dola 1000  na kiwango cha chini cha ziada ni Dola 100 huku muda wa kuweka bila kutoa ikiwa ni siku 90.