Diwani, mkewe wafariki ajalini Tabora

Muktasari:

  • Diwani huyo na mkewe walikuwa wakitoka nyumbani kwao Kata ya Kalola kuja Tabora mjini na ndipo gari lao lilipogongana uso kwa uso na gari lingine na wao kufariki papo hapo.

Tabora. Diwani wa Kata ya Kalola wilayani Tabora (Uyui), Sauji Daud na mkewe, Magdalena Richard wamefariki dunia katika ajali ya gari usiku wa kuamkia leo Jumanne Oktoba 25, 2022.

Akizungumza na Mwananchi leo, Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo, Said Ntahondi amesema, diwani huyo na mkewe walikuwa katika gari yao binafsi wakitoka Kalola kuja Tabora mjini na ndipo gari lao lilipogongana na gari lingine uso kwa uso na wao kufariki papo hapo.

Amesema miili yao imepelekwa kuhifadhiwa hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Tabora, Kitete kwa ajili ya uchunguzi na taratibu zingine.

"Tunasubiri uchunguzi na taarifa nyingine za wana ndugu kabla ya kupanga mazishi yao," amesema.