Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Diwani wa Chadema Muheza atimkia CCM

Aliyekuwa Diwani wa Chadema Kata ya Mkuzi George Chambai. Picha na Raisa Said

Muheza. Diwani wa Kata ya Mkuzi Wilaya ya Muheza mkoani Tanga, George Chambai kwa tiketi ya  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) amejiunga rasmi na Chama cha Mapinduzi CCM leo Jumapili Septemba 10, 2023.

Ametangaza kuachana na chama chake cha zamani wakati wa Mkutano wa hadhara wa CCM  uliofanyika viwanja vya Sokoni Mkuzi nakuhudhuriwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa  wa Tanga, Rajab Abrahaman na Mbunge wa Muheza, Hamis Mwinjuma maarufu ‘Mwana FA’ na viongozi wengine wa chama na Serikali.

Chambai amesema kuwa hakushawishiwa na mtu yeyote katika uwamuzi wake, bali amefanya hivyo baada ya kuridhishwa na kasi ya maendeleo inayofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan.

"Nimehama kwa mapenzi yangu, siasa siyo chuki wala ugomvi, tunataka watu wapate maendeleo  ya haraka hivyo sikuwa na sababu ya kubaki upinzani,"amesema.

Akizungumza katika mkutano huo, mwenyekiti wa CCM Rajab Abrahaman amempongeza Diwani huyo kuamua kujiunga na chama cha mapinduzi na kwamba ameahidi watampa ushirikiano wa kutosha .

Mwenyekiti huyo ameongeza ifikapo mwakani wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa, CCM mkoani Tanga haitafanya mzaha na kwamba watahakikisha inashinda nafasi zote za uongozi.

Ameongeza mkoa huo umejipanga kuhakikisha unaongoza kitaifa katika kumpa kura nyingi Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan wakati wa uchaguzi mkuu ujao,  pia wanashinda kata zote 245, vijiji, vitongoji na Mitaa yote mkoani Tanga.