Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dk Bashiru amuombea msamaha Makonda

Muktasari:

Katibu mkuu wa CCm, Dk Bashiru Ally amesema kutokana na kutofanyika kwa kazi ya kuandaa viongozi bora matunda ya kutoandaa vijana yameanza kuonekana.

Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally amesema kutokana na kutofanyika kwa kazi ya kuandaa viongozi bora matunda ya kutoandaa vijana yameanza kuonekana.

Ameyasema hayo leo Alhamisi ya Mei 9, 2019 katika ibada ya mazishi ya Mwenyekiti wa kampuni za IPP, Reginald Mengi inayofanyika katika kanisa la KKKT Usharika wa Moshi mjini.

“Kuwa viongozi bora, watiifu, wanyenyekevu na wenye heshima, naomba nitumie fursa hii kumuombe msamaha kijana wangu Makonda mimi namfahamu na hii ni mara yangu ya pili namsema hadharani,”

“Mara yangu ya kwanza nilimsema Simiyu akaja analia ofisini nikasema ubadilike na kwa kweli ameanza kubadilika, bado ni kijana mzuri, shupavu lakini tunahitaji kuwasaidia vijana wetu,” amesema Dk Ally

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kitendo cha Dk Bashiru kuomba radhi kwa niaba yake ni upendo wa hali ya juu lakini alibainisha kuwa huenda trafsiri ya maneno aliyoyatoa hayakueleweka vizuri.

“Mimi niombe radhi kwa tafsiri hiyo kwa sababu nimemsifia mchaga katikati ya wachanga siyo mchaga katikati ya kabila lingine, mapokeo na nitaendelea kumuenzi mzee Mengi kwa mema yote aliyoyafanya kwa walemavu hasa katika mkoa wetu yatabaki kuwa alama,” amesema Makonda