Dk Hoseah rais mpya TLS

Dk Hoseah rais mpya TLS

Muktasari:

  • Mkurugenzi wa zamani wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hoseah amechaguliwa kuwa rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS).

Arusha. Mkurugenzi wa zamani wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hoseah amechaguliwa kuwa rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS).

Ameibuka mshindi kwa kura 297 katika uchaguzi huo uliofanyika jijini Arusha leo Ijumaa Aprili 16, 2021 na kuwashinda washindani wake wanne.

Katika uchaguzi huo Flaviana Charles alipata kura  223, Shehzad Wall (192), Albert Msando (69) na rais wa zamani wa chama hicho, Francis Stola akiambulia kura 17.