Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dk Kitine: Nitairudisha Tanzania ya Mwalimu Nyerere

> Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa wa zamani, Dk Hassy Kitine akizungumza katika Ukumbi wa Royal Village mjini Dodoma jana alipokuwa akitangaza nia ya kukiomba Chama Cha Mapinduzi (CCM) kumteua kuwa mgombea wa Urais kupitia chama hicho katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu. Picha na Edwin Mjwahuzi

Muktasari:

Kitine alitangaza nia hiyo jana mjini Dodoma akitumia sehemu kubwa ya hotuba yake kutoa mifano ya utendaji wa muasisi huyo wa Taifa, huku akiwaponda waliotangaza nia wengine na kujisifu kuwa hakuna mwenye sifa za kumfikia, hasa katika elimu.

Dodoma. Mkurugenzi mkuu wa zamani wa Idara ya Usalama wa Taifa, Dk Hassy Kitine, ametangaza nia ya kugombea urais kwa tiketi ya CCM, akisema “nipeni miaka mitano niirudishe Tanzania ya Mwalimu (Julius) Nyerere”.

Kitine alitangaza nia hiyo jana mjini Dodoma akitumia sehemu kubwa ya hotuba yake kutoa mifano ya utendaji wa muasisi huyo wa Taifa, huku akiwaponda waliotangaza nia wengine na kujisifu kuwa hakuna mwenye sifa za kumfikia, hasa katika elimu.

“Ninataka kuirudisha Tanzania ya Mwalimu Nyerere… sikuwahi kutangaza wala kuonyesha dalili zaidi ya kukaa na kutafakari katika nafsi… najua sitaweza kufanya kama alivyokuwa Mwalimu, lakini nitasimamia katika misingi ya utendaji ya Mwalimu Nyerere,” alisema waziri huyo wa zamani.

Alisema kuwa enzi za uhai wa Mwalimu Nyerere aliwahi kusema “Ikulu si pa kukimbilia, Ikulu ni shida, Ikulu ni matatizo”, akisisitiza kuwa ofisi hiyo ya mkuu wa nchi ni matatizo na hata yeye anaiogopa.

“Mwalimu alisema ‘ukiona mtu anakimbilia Ikulu kwa namna yoyote ile, na hasa kwa mapesa, mapesa siyo fedha, mapesa, mapesa, mapesa mpaka yanatisha. Huyu mtu akienda Ikulu lazima azirudishe, na (Ikulu) si pa biashara. Sasa anakwenda kufanya biashara gani?’

“Huyu ni wa kuogopa kama ukoma…mimi ninaijua Ikulu kuliko mgombea mwingine yeyote. Nilikuwa Ikulu kama kiongozi, kila mlango wa chumba Ikulu naujua, hata alipolala Baba wa Taifa. Ikulu si pa kukimbilia.

“Nimefanya kazi Ikulu kwa muda mrefu sana, Ikulu ni shida… ninazijua Ikulu zote Tanzania, si pa kukimbilia, Ikulu ni matatizo, matatizo, matatizo. Sasa pamoja na matatizo hayo, nimewiwa kuchukua fomu kwa kuwa sikuona hata anayefaa kati ya waliochukua,” alisema Kitine.

“Wanahangaika kwenda Ikulu, wanahangaika kwelikweli. Wapo waliotangaza nia na kujaza viwanja vya mpira, wanajaza watu, wanafanya mbwembwe. Sasa nikaangalia hivi kweli hawa wanataka kulitumikia Taifa kwa mbwembwe zote hizi au wanataka kurudisha fedha zao?

“Ndiyo maana nikaogopa sana na nimejitokeza mwishomwisho kwa kuwa Ikulu napafahamu sana, si kidogo, sikukimbilia. Naona tabu hata nikichaguliwa, naogopa kwelikweli, kwa sababu najua kuna matatizo sana.”

Alisema akiwa Ikulu na akiwa na miaka 30 aliteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, alikataa lakini Nyerere alimlazimisha, hivyo akamwambia waendelee na watasaidiana.

“Leo ninatangaza nia hapa badala ya Makete. Watanisamehe huko, wapo waliofanyia nyumbani na maeneo yao, lakini mimi naona ni usanii usanii tu. Wanajaza watu lakini kumbe hakuna lolote ni mambo ya hela na rushwa tu,” alisema.

“Mimi nawaambia, wakiwapa pesa chukueni, kwanza kwa kuwa hakuna anayekataa fedha, pili, fedha hizo wamewaibia ninyi, na wanawarudishia kwa njia hiyo,” alisema Kitine huku akisema kuwa anaumizwa na kitendo cha kuitwa mwizi alipokuwa mtumishi wa umma wakati yeye mwadilifu.

“Waliniita mwizi, waziri mwizi,” alisema.

Kitine alivishukia vyombo vya habari akisema kuwa kutokana na mbinu za Usalama wa Taifa anajua baadhi vimenunuliwa na baadhi ya wagombea ili kupiga kampeni, huku akisema kuwa wakitoa fedha wale lakini wasiwape kura.

“Msije mkawapa kura kwa kuwa kura yako haina thamani ya fedha unayopewa hata Sh10, Sh50,000, shilingi milioni, kura yako ina thamani kubwa sana,” alisema.

“Kura yako siyo pesa, kura ni usalama wa maisha yako, kura kwa mlinzi wa maisha yako, mlinzi wa familia yako. Msiwapitishe hawa, sasa usalama wako ni shilingi ngapi?.”

Alisisitiza kuwa Watanzania wasiwape kura wanaohonga kwa ajili ya Ikulu, lakini akawaomba radhi kama amewagusa baadhi.

Hadi sasa takriban makada 30 wameshajitokeza kuchukua fomu au kutangaza nia ya kuomba ridhaa ya CCM ili wapitishwe kugombea urais, kitu ambacho Kitine anaona kuwa ni kama kuinunua Ikulu ndiyo maana kila mmoja anaitamani.

Kuhusu mpango wake wa kuirudisha Tanzania ya Mwalimu Nyerere,Kitine alisema pia kuwa akipata ridhaa, ataboresha raslimali na maisha ya Watanzania.

Alitaja mambo 12 yanayompasa Rais wa kuongoza Tanzania akisema yeye ndiye anayefaa na ana sifa zote za kushika nafasi hiyo.

Alitaja sifa hizo kuwa ni mtu mwenye uwezo wa kuangalia usalama wa Taifa, uwezo na utashi wa ulinzi wa Taifa, sanjari na mipaka yake, kwa kuwa kuna watu wengi wanaingia sasa hivi na kufanya mambo wanayoyajua, na tatu mtu mwadilifu wa asili tangu kuzaliwa.

Kwa mujibu wa Kitine, sifa ya nne ya rais ni elimu ya kutosha na si lazima asome sana kama yeye na kutamba kuwa amesoma zaidi ya makada wengine waliotangaza nia ya kuutaka urais.

Alisema ya tano ni kuifahamu Tanzania akisema kuwa yeye anaifahamu nchi kutokana na mazingira bya kazi yake yaliyomlazimisha kupita kila kona kiasi cha kuzijua alama zote za mipaka ya Tanzania.

Sifa ya sita kwa mujibu wa Dk Kitine ni kuwa na sera sahihi za maendeleo ya Tanzania kama kilimo, viwanda, uchukuzi, afya, elimu na kujujua maisha ya Watanzania.

Ya saba alisema ni uwezo wa kutoa uamuzi mgumu, kutoshadidia vitu visivyo na tija na mwenye nia na uwezo wa kupambana na rushwa.

Sifa ya nane aliitaja kuwa ni kuchukia rushwa kwa dhati, na kuonekana kuwa na dhamira ya dhati na ya tisa ni kuwa mwoga wa kukiuka sheria, mwenye kuzisimamia sheria, akisema Tanzania ina sheria nyingi, lakini hazifuatwi, hata sheria ya kutupa taka lakini hakuna wa kuzisimamia.

Alisema sifa ya kumi ni kuwa mtu mwenye kumuogopa Mungu na ajitahidi kumwogopa Mungu, wakati aliitaja sifa ya 11 kuwa ni kiongozi mwenye tabia ya kuwapenda Watanzania, akisema ndio watakaomlilia.

Dk Kitine alitaja sifa ya mwisho kuwa ni kujua mgawanyo sawa wa mali, licha ya kuwepo kwa changamoto nyingi.

Hata hivyo, alisema kuwa Tanzania ina changamoto nyingi zinazohitaji utatuzi, likiwemo suala la rushwa.

Kitine aligusia suala la uadilifu, kwamba pamoja na matatizo hayo ndani ya CCM, hata watumishi wa Serikali wamekosa uadilifu, na hali hiyo inaonekana kwa Afrika.

Alisema viongozi wa Afrika wamekosa uadilifu na kwamba wengi wana tamaa ya madaraka, lakini akasema yeye yuko radhi miaka mitano tu apewe ili aiweke Tanzania kwenye mstari wa Mwalimu Nyerere.

Akizungumzia uhuru wa habari na muswada wa sheria ya habari, Dk Kitine alisema kwanza anakerwa na mfumuko wa magazeti kwamba ni mengi mno na wakati mwingine yanachanganya wasomaji huku akisema ataifanyia kazi sheria ya vyombo vya habari, kwamba akiingia madarakani ataipitia aone kasoro zilizopo.

Kuhusu kuporomoka kwa shilingi na nafasi yake katika urais, alisema kuwa akiingia madarakani, ataelekeza nguvu katika kilimo, uzalishaji mali na kufufua viwanda kwa ajili ya kuuza mazao ya biashara ili kuiokoa shilingi zaidi ya kuuza mazao ghafi.

Vilevile alisema kuwa akiingia madarakani atawafuatilia wote wanaojiita wasomi ‘feki’ kuangalia kama kweli wamepata sifa hiyo na wakithibitisha kuwa na makosa watafikishwa mahakamani.

“Hapa kila mtu anaitwa dokta, dokta, dokta… wengine udaktari wao wameupata kwenye mtandao. Nitaleta sheria ya kuwachunguza na wakibainika tutawafunga,” alisema.

Kitine ni nani?

Dk. Hass Kitine alizaliwa mwaka 1943 katika Kijiji cha Kisinga, Kata ya Lupalilo, Tarafa ya Lupalilo, Wilaya ya Makete. Mwaka 1950 alianza Shule ya Msingi ya Rungwe, Tukuyu.

Mwaka 1954 akafaulu kwenda Shule ya Kati ya Ndembela na 1958 alifaulu kutoka Ndembela kwenda Shule ya Sekondari Malangali ambako alihitimu darasa la 12 mwaka 1961.

Baada ya kufaulu mtihani wa Cambridge mwanzoni mwa mwaka 1962 alipelekwa Tabora Boys. Mwaka 1964 alifaulu kwenda Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) kusoma Shahada ya uchumi. Baada ya kuhitimu alianza kazi ya ualimu katika Shule ya Sekondari Ihungo iliyoko Bukoba mkoani Kagera.

Mwaka 1969 alijiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Ruvu, kwa mujibu wa sheria. Hakupenda kubaki JKT hivyo akaamua kujiunga na Jeshi la Wananchi, akianzia mafunzo ya awali Mgulani na baadaye kupelekwa Uingereza na aliporejea akapata cheo cha luteni usu.

Mwaka 1971 akiwa na cheo cha luteni, alipelekwa kufanya kazi Nachingwea, akiwa kamanda wa platuni ambako alikisaidia chama cha Freelimo kilichokuwa kinapigania uhuru wa Msumbiji.

Mwaka 1971 aliteuliwa kuwa afisa msaidizi wa mafunzo wa JWTZ , pia aliwahi kuwa ofisa elimu wa siasa 1972, kisha akapelekwa Monduli ambako Aprili 1974 alirejeshwa Dares Salaam kuwa msaidizi wa mkuu wa majeshi, kama Katibu wa Mkuu wa Majeshi. Baadaye akahamishiwa mkoani Morogoro kwenye kiwanda cha kutengeneza silaha ndogo, akiwa naibu meneja mkuu na baadaye kuteuliwa kuwa mkuu wa Chuo cha Monduli

Mwezi Februari mwaka 1976, Rais alimteua kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa. Mwaka 1986 alitunukiwa Shahada ya Uzamili kutoka Chuo cha Lakehead na 1993 alitunukiwa Shahada ya Uzamivu katika Chuo cha Simon Fraser.

Akiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora) katika Serikali ya Rais Benjamin Mkapa, Dk Kitine alilazimika kujiuzulu baada ya kutuhumiwa kushirikiana na mkewe, kufanya udanganyifu na hatimaye Serikali ikatoa fedha za umma kiasi cha Dola za Marekani 50,000, kwa ajili ya mkewe kwenda kutibiwa Marekani wakati hakuwa mgonjwa.

Uzoefu wake kiuongozi

Kati ya mwaka 1997 na 2005, Dk Kitine alikuwa mbunge katika Bunge la Jamhuri ya Muungano na mwaka 2000 hadi 2005 alikuwa Mbunge wa Afrika Mashariki.

Pia amekuwa mkufunzi wa masuala ya uchumi katika vyuo vikuu mbalimbali, ikiwamo Canada na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Kitine alitangaza nia hiyo jana mjini Dodoma akitumia sehemu kubwa ya hotuba yake kutoa mifano ya utendaji wa muasisi huyo wa Taifa, huku akiwaponda waliotangaza nia wengine na kujisifu kuwa hakuna mwenye sifa za kumfikia, hasa katika elimu.

“Ninataka kuirudisha Tanzania ya Mwalimu Nyerere… sikuwahi kutangaza wala kuonyesha dalili zaidi ya kukaa na kutafakari katika nafsi… najua sitaweza kufanya kama alivyokuwa Mwalimu, lakini nitasimamia katika misingi ya utendaji ya Mwalimu Nyerere,” alisema waziri huyo wa zamani.

Alisema kuwa enzi za uhai wa Mwalimu Nyerere aliwahi kusema “Ikulu si pa kukimbilia, Ikulu ni shida, Ikulu ni matatizo”, akisisitiza kuwa ofisi hiyo ya mkuu wa nchi ni matatizo na hata yeye anaiogopa.

“Mwalimu alisema ‘ukiona mtu anakimbilia Ikulu kwa namna yoyote ile, na hasa kwa mapesa, mapesa siyo fedha, mapesa, mapesa, mapesa mpaka yanatisha. Huyu mtu akienda Ikulu lazima azirudishe, na (Ikulu) si pa biashara. Sasa anakwenda kufanya biashara gani?’

“Huyu ni wa kuogopa kama ukoma…mimi ninaijua Ikulu kuliko mgombea mwingine yeyote. Nilikuwa Ikulu kama kiongozi, kila mlango wa chumba Ikulu naujua, hata alipolala Baba wa Taifa. Ikulu si pa kukimbilia.

“Nimefanya kazi Ikulu kwa muda mrefu sana, Ikulu ni shida… ninazijua Ikulu zote Tanzania, si pa kukimbilia, Ikulu ni matatizo, matatizo, matatizo. Sasa pamoja na matatizo hayo, nimewiwa kuchukua fomu kwa kuwa sikuona hata anayefaa kati ya waliochukua,” alisema Kitine.

“Wanahangaika kwenda Ikulu, wanahangaika kwelikweli. Wapo waliotangaza nia na kujaza viwanja vya mpira, wanajaza watu, wanafanya mbwembwe. Sasa nikaangalia hivi kweli hawa wanataka kulitumikia Taifa kwa mbwembwe zote hizi au wanataka kurudisha fedha zao?

“Ndiyo maana nikaogopa sana na nimejitokeza mwishomwisho kwa kuwa Ikulu napafahamu sana, si kidogo, sikukimbilia. Naona tabu hata nikichaguliwa, naogopa kwelikweli, kwa sababu najua kuna matatizo sana.”

Alisema akiwa Ikulu na akiwa na miaka 30 aliteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, alikataa lakini Nyerere alimlazimisha, hivyo akamwambia waendelee na watasaidiana.

“Leo ninatangaza nia hapa badala ya Makete. Watanisamehe huko, wapo waliofanyia nyumbani na maeneo yao, lakini mimi naona ni usanii usanii tu. Wanajaza watu lakini kumbe hakuna lolote ni mambo ya hela na rushwa tu,” alisema.

“Mimi nawaambia, wakiwapa pesa chukueni, kwanza kwa kuwa hakuna anayekataa fedha, pili, fedha hizo wamewaibia ninyi, na wanawarudishia kwa njia hiyo,” alisema Kitine huku akisema kuwa anaumizwa na kitendo cha kuitwa mwizi alipokuwa mtumishi wa umma wakati yeye mwadilifu.

“Waliniita mwizi, waziri mwizi,” alisema.

Kitine alivishukia vyombo vya habari akisema kuwa kutokana na mbinu za Usalama wa Taifa anajua baadhi vimenunuliwa na baadhi ya wagombea ili kupiga kampeni, huku akisema kuwa wakitoa fedha wale lakini wasiwape kura.

“Msije mkawapa kura kwa kuwa kura yako haina thamani ya fedha unayopewa hata Sh10, Sh50,000, shilingi milioni, kura yako ina thamani kubwa sana,” alisema.

“Kura yako siyo pesa, kura ni usalama wa maisha yako, kura kwa mlinzi wa maisha yako, mlinzi wa familia yako. Msiwapitishe hawa, sasa usalama wako ni shilingi ngapi?.”

Alisisitiza kuwa Watanzania wasiwape kura wanaohonga kwa ajili ya Ikulu, lakini akawaomba radhi kama amewagusa baadhi.

Hadi sasa takriban makada 30 wameshajitokeza kuchukua fomu au kutangaza nia ya kuomba ridhaa ya CCM ili wapitishwe kugombea urais, kitu ambacho Kitine anaona kuwa ni kama kuinunua Ikulu ndiyo maana kila mmoja anaitamani.

Kuhusu mpango wake wa kuirudisha Tanzania ya Mwalimu Nyerere, Kitine alisema pia kuwa akipata ridhaa, ataboresha rasilimali na maisha ya Watanzania.

Alitaja mambo 12 yanayompasa Rais wa kuongoza Tanzania akisema yeye ndiye anayefaa na ana sifa zote za kushika nafasi hiyo.

Alitaja sifa hizo kuwa ni mtu mwenye uwezo wa kuangalia usalama wa Taifa, uwezo na utashi wa ulinzi wa Taifa, sanjari na mipaka yake, kwa kuwa kuna watu wengi wanaingia sasa hivi na kufanya mambo wanayoyajua, na tatu mtu mwadilifu wa asili tangu kuzaliwa.

Kwa mujibu wa Kitine, sifa ya nne ya rais ni elimu ya kutosha na si lazima asome sana kama yeye na kutamba kuwa amesoma zaidi ya makada wengine waliotangaza nia ya kuutaka urais.

Alisema ya tano ni kuifahamu Tanzania akisema kuwa yeye anaifahamu nchi kutokana na mazingira ya kazi yake yaliyomlazimisha kupita kila kona kiasi cha kuzijua alama zote za mipaka ya Tanzania.

Sifa ya sita kwa mujibu wa Dk Kitine ni kuwa na sera sahihi za maendeleo ya Tanzania kama kilimo, viwanda, uchukuzi, afya, elimu na kujua maisha ya Watanzania.