Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

FYATU MFYATUZI: Fyatu afaidi IEFUDI kwa raha zake mwenyewe!



Juzi, nikiwa napata kalaji si nikajifunza kitu. Kwanza, nilikasirika nusu niue fyatu. Nilichanganyikiwa hadi nikachanganyikana! Nikiwa ndo nimerudi kupata, si akaja afisa wa mamlaka ya kuibiana. Kumbe kuna jirani yangu mnoko alinichoma.

Si niliuza vikuku vitatu tena kwa bei ya kutupa. Loh! Jamaa kanijia nyumbani eti kutaka nimuonyeshe IEFUDI. Nilimuuliza IEFUDI ni mnyama gani.

Hakujibu zaidi ya kunitisha kuwa lisrikali litakamata kuku wangu waliobaki hadi nionyeshe IEFUDI. Bila ajizi, nilimuomba naye anipe hiyo IEFUDI yake kama siyo ukosefu wa ubunifu, ujambazi na wizi vya kichovu.

Kwa uzwazwa wake alinijibu kuwa mie nilikuwa nani kumkatisha IEFUDI wakati yeye ndiye hiyo IEFUDI.

Nilizidi kumchanganya. Niliuliza hilo lisrkali lake mbona halituonyeshi IEFUDI linapopata misaada na kukopa likaihomola na kuondomola. Niizidi kumzonga anieleze nielewe kama wapigaji wa njuluku ndefu inayofichuliwa kila mwaka na KAG (Kagua, Aibisha, na Kuufyata), nao, wana hiyo IEFUDI.

Jamaa zwazwa kweli. Si lilianza kupayuka utadhani kaya ya Fyatuland ni mali ya baba au mama yake. Baada ya kuona rongorongo zimezidi, nililipiga mkwara kwa kupiga simu ya mshirika wangu wa bedroom nikijidai ni mwanasheria wangu ili alishitaki na waliolituma.

Huu ujambazi na wizi wa mchana umeniudhi sana. Mbona pale kwa Gabacho wanauza bidhaa zilizoisha muda wa matumizi. Je, hawa wa IEFUDI hawaoni haya au wanatuchukulia ufala na uzwazwa?

Nani hajui kuwa Fyatuland ishauzwa zamani gani au wanataka kutuuza baada ya kutuchuuza? Mbona misongamano imezidi hadi makaburini? Je, kazi ya lisrikal ni nini au ni kutupiga Mafyatu wachovu?

Kweli, wamejua kututenda na kututenza. Kuanzia leo, nataka kujua mwenye kaya kati ya wanakaya na walakaya ili kijulikane. Kama mbaya mbaya.

Fyatu anaanzisha genge. Kila jizi, tena bila aibu wala adabu linakuja kudai sijui tozo la nini, sijui IEFUDI sijui utopolo na upuuzi gani. Je, namna hii twaweza kuendelea au kuendelea katika kutoendelea?

Ngoja nizoze kiprofesoo. Hivi, tumeishiwa hivi kiasi cha kuhangaishwa na mafyatu wadogo na vitu vidogo wakati uchumi tunao tunaukalia na wachukuaji wanakuja na kujizolea? Je, Fyatuland siyo shamba la bibi tena bibi mwenye kipofu na taahira? Basi, tubadili jina iitwe Shambalabibiland kijulikane. Ajabu ya maajabu, hii mijizi inayokuja kutunyima raha haijui hata hiyo njuluku inatafutwaje. Kazi, kuja kutughasi na kutuibia. Nasi Mafyatu tuna dhambi.

Kwanini tunakubali wizi huu wa nchana? Hii njuluku wanayozoa na kupiga wanaifanyia nini? Kazi yao ni nini au wanatugeuza kuku na mbuzi? Kwanini tujirahisi na kukubali kunyonywa hivi na chawa, kunguni, funza, luba, na wadudu wengine ambao siku hizi wamenenepeana wakati twakondeana? Hivi, nani alituroga hadi tukajihisi wageni kwetu?
 Hapa, naongelea IEFUDI. Bado madude mengine ya kimchoromchoro yaliyotamalaki. Ajabu, haya machawa na ma IEFUDI yanayotunyonya na kutuuma yanajiita matumishi ya umma!

Ni matumishi ya umma au ya kuuma Mafyatu? Kama unaona mimi kufuga vijikuku vitatu na kuuza nawe ukanijia na hizo IEFUDI zako, jaribu ufuge uone cha moto.

Huwa siachi kuudhika na kushangaa. Hii soma kimya kimya. Juzi, si kuna changu kaniuzia dhambi zake. Baada ya kumaliza kanchezo si alitaka nimpe ujira wake.

Sikupinga wala kubisha. Nilimtaka anipe IEFUDI yake ili nimlipe na kunipatia risiti. We! Hilo zegere, usipime. Dada wa watu alinifyatukia na kunitukana mitusi ya nguoni kama hakuwa na akili nzuri.

Baada ya kumalizana aliponitishia angekwenda kudai kwa bi Mkubwa wangu, nilimlipa na kutoka nduki kama kibaka aliyekwapua cheni pale Migomigo. Tuache utani. Kama ni hivyo, ili kutenda haki, na wala rushwa wakipokea mlungura lazima nao wawe na IEFUDI s na kutoa risiti.

Badala ya kudai haki eti tunafundishwa kudai risiti wakati wanaosimamia hizo risiti nao haawatoi risiti. Uko wapi usawa na haki hapa au navyo vinaendelea kuwa machukizo mbele ya majizi wanene?

Pamoja na kuichukia IEFUDI, siku hizi naanza kuipenda badala ya kuiponda. Kwani, nakata kanywaji bila kulipa. Nikiletewa vyupa, navipiga kwa raha zangu.

Baada ya hapo, akija muuzaji, namtakisha IEFUDI ili anipe risiti. Hivyo, hivyo, nimepiga kalaji dezo hadi wauza wakagutuka. Siku hizi, nikiingia tu na kuagiza, wanataka nilipe kwanza. Huwa nawatakisha IEFUDI. Maskini wengi hawajui hata hiyo IEFUDI ni nini! Hata niendapo kwenye vyoo za kulipia, huwa nadai wanipe IEFUDI. Huu ndiyo uzuri wa IEFUDI kwa wajanja kama mimi.

Hayo tuyaache. Kama ni lazima kuwa na IEFUDI s, basi, na wanene watoe risiti wanapokwapua njuluku za Mafyatu waliogoma kufyatuka wakawafyatua wanaowafyatua kila uchao. Bila kufyatuka na kufyatua, Mafyatu watafyatuliwa hadi waone kaburi.

Hivi, hawa wanaotuuzia ulabu, nao wanazo IEFUDI? Haya si mmbo ya nchezo wala uchonganishi na uchocheaji bali jiani iliyohalalishwa na kuwa nyenzo ya wachache kutupiga na kutuumiza. Kesho, mtatwambia tutoe hata risiti za marehemu wetu waliozikwa miaka mingi iliyopita.

Sina ugomvi na kukusanya njuluku na mapato. Je, Mafyatu wananufaika vipi na hayo mapato wakati kila mwaka KAG anaibua kashfa ya upigaji wa njuluku ndefu na majizi hayakamatwi wala kushitakiwa? Hapa, hatujaliwa tukijiona kweli? Tunahitaji sana kufanya mapinduzi ya kifikra. Hivi, naota au naweweseka!!!