Dk Mdolwa aambulia kura 64 CCM, asema “sio haba”

Aliyekuwa mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Dk Edmund Mndolwa

Muktasari:

Mwenyekiti aliyepita katika Jumuiya ya Wazazi Taifa Dk Edmund Mndolwa amesema kura 64 alizopata sio haba.

Dodoma. Aliyekuwa mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Dk Edmund Mndolwa amesema kura 64 alizopata sio haba.

  

Mndolwa alishindwa kutetea kiti chake katika uchaguzi wa Jumuiya ya Wazazi Taifa uliofanyika jana Novemba 24, 2022 jijini Dodoma.


Katika uchaguzi huo, Fadhil Maganya aliibuka mshindi kwa kupata kura 578 kati ya 835 huku Dk Mndolwa akipata kura 64.


Akizungumza baada ya Mwenyekiti mpya Maganya kumpa nafasi Dk Mndolwa aliwashukuru wajumbe kwa kumpigia kura hizo.


"Nimepata kura 64 sio haba hilo sio tatizo kikubwa tumepata viongozi wapya tuwasapoti," amesema Dk Mndolwa.


Pia alitumia nafasi hiyo kuwashukuru wale wote aliofanya nao kazi katika kipindi cha miaka mitano.


"Nashukuru sana nataka nimpongeze Mwenyekiti kwa kuchaguliwa Jumuiya hii ni kongwe inaweza kuisaidia Chama na Serikali,” amesema Dk Mndolwa.