Dk Mpango aelezea alimvyomfahamu Ole Nasha

Makamu wa Rais Dk Philip  Mpango akimfariji  Asha Mlekwa mke wa marehemu William Ole Nasha aliyekuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu  Uwekezaji alipofika nyumbani kwa marehemu Medeli jijini Dodoma.

Muktasari:

  •  Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk Philip Mpango amemuelezea aliyekuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezajii), William Ole Nasha kuwa alikuwa kiongozi hodari na asiye na makuu.

 .


Dodoma. Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk Philip Mpango amemuelezea aliyekuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), William Ole Nasha kuwa alikuwa kiongozi hodari na asiye na makuu.

Ole Nasha alifariki dunia usiku Jumatatu Septemba 27, 2021  shughuli za kuaga mwili wake zitafanyika kesho katika viwanja vya Bunge kabla ya kusafirishwa kwenda kijijini kwao Ngorongoro.

Dk Mpango ameeleza hayo leo Jumatano Septemba 29, 2021 alipofika kutoa pole kwa familia nyumbani kwa Ole Nasha eneo la Medeli jijini hapa.

Makamu wa Rais amesema mara ya mwisho alikutana na Ole Nasha Septemba 22, mwaka huu alipoalikwa na waziri wa Viwanda kwenda kufungua maonyesho ya shirika la kuhudumia viwanda vidogo (Sido)  Wilaya Kisulu mkoani Kigoma.

Amesema siku hiyo walifanya shughuli hiyo pamoja na kuzungukia, kukagua mabanda pamoja na kuzungumza na wananchi na wala hakuonesha dalili yoyote ya kuuumwa.

“Nina uhakika manaibu waziri wenzake na mawaziri aliowasaidia wote wanamsemea mema kama wengine wote tunavyomshuhudia,”amesema na kuongeza;

“Wanangorongoro wamepoteza kiongozi mahiri sana.”

Imeandikwa Alex Deodatus na Salim Abubakary, Tudarco