Dk Mpango ataja zawadi ya Rais Samia kwa Watanzania

Muktasari:

  • Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk Philip Mpango amesema kitendo cha Rais Samia Suluhu Hassan kukutana na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa nchini ni zawadi ya mwaka mpya 2023.

Dar es Salaam. Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk Philip Mpango amesema kitendo cha Rais Samia Suluhu Hassan kukutana na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa nchini ni zawadi ya mwaka mpya 2023.

Hayo ameyasema leo Jumanne, Januari 3, 2023 Ikulu jijini Dar es Salaam akisisitiza hatua hiyo ya Rais Samia utekelezaji wa maagizo ya hayati Rais wa kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere.

"Amefata msisitizo wa Hayati Mwalimu Julius Nyerere ya nchi kujengwa kwa umoja uzalendo kwa maslahi ya Tanzania, hii ni zawadi nzuri ya kufungulia mwaka 2023," amesema.

Kwa upande wake, Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi amesema vyama vyote 19 vimewatuma wawakilishi katika mkutano huo.

 Amesema kitendo cha viongozi hao kufika kwa wingi ni dalili nzuri ya kuingia mwaka mpya akisisitiza hiyo ni dalili njema.

"Ahadi yangu tutafanya kazi kwa weledi na moyo mliyoonyesha tuheshimu na kufuata sheria zilizopo mapungufu yaliyopota mwaka uliopita siyo tutakayoenda nayo mwaka huu,” amesema

Amemwomba Rais Samia  mapungufu ya sheria yaliyopo ayafanyie kazi.

Mkutano huu wa Rais Samia ni wa kwanza ukiwa na sura ya kitaifa ambapo viongozi wakuu wote wa vyama vya upinzani hasa chama kikuu cha upinzani Chadema kikihudhuria.

Ikumbukwe Desemba 2021 jijini Dodoma, Rais Samia alikutana na vyama na wadau wa siasa lakini mkutano huo ulisusiwa  na Chadema na NCCR-Mageuzi.

Hata hivyo, mwelekeo wa sisa nchini ulianza kuonekana kuwa na matumaini baada ya kiongozi mkuu wa Chadema, Freeman Mbowe aliyeshitakiwa kwa ugaidi kufutiwa mashitaka hayo.

Kitengo cha kiongozi huyo kufanya mazungumzo mara kwa mara na Rais Samia