Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dk Mpango kufungua mkutano wa korosho Dar

Muktasari:

  • Zaidi ya wadau 500 kutoka nchi 33 zinazozalisha na kula korosho, wanatarajia kushiriki katika mkutano wa kimataifa wa zao hilo nchini utakaoanza Oktoba 11 hadi 13, 2023 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JKNICC) kilichopo jijini Dar es Salaam.

Mtwara. Zaidi ya wadau 500 kutoka ya nchi 33 zinazozalisha na kula korosho, wanatarajia kushiriki katika mkutano wa kimataifa wa zao hilo nchini utakaoanza Oktoba 11 hadi 13, 2023 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JKNICC) kilichopo jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho nchini, (CBT) ameyasema leo Oktoba 5, 2023 kuwa Makamu wa Rais, Philip Mpango anatarajia kuwa mgeni rasmi wa mkutano huo.

Alfred amesema mkutano huo umeandaliwa kwa ushirikiano wa CBT, Kituo cha uwekezaji nchini, (TIC), Kituo cha Utafiti wa Kilimo nchini, (TARI) Naliendele pamoja na wadau wengine.

Pamoja na mambo mengine, lengo la mkutano huo amesema ni kutangaza fursa za uwekezaji zilizoko katika mnyororo wa thamani wa zao la korosho.

“Mkutano huu ni fursa kwa Watanzania ya kukutana na wadau mbali mbali pia kutakuwa na mada mbali mbali za mnyororo wa zao la korosho, uzalishaji, teknolojia zinazotumika na wenzetu na hapa nchini” amesema Alfred.

Vile vile kutakuwa na mada juu ya namna gani wanaweza kutumia teknolojia ya kidigitali katika uzalishaji kuanzia shambani hadi sokoni na upatikanaji wa fedha au mitaji katika zao hilo na mwenendo wa soko la korosho.

Katika msimu wa mwaka huu 2023/2024 unaotarajia kuanza Oktoba 20, 2023  matarajio ni kuzalisha tani 400,000 za korosho kitaifa.

Msimu uliopita malengo yalikuwa kuzalisha Tani hizo 400,000 lakini tani 285,000 zilizalishwa.

Mkutano huu unakuja ikiwa ni siku chache kabla ya kuanza kwa msimu wa korosho mwaka huu 2023/2024 unaotarajia kuanza Oktoba 20, 2023.

Katika ziara yake mkoani hapa hivi karibuni, Rais Samia Suluhu Hassan aliagiza korosho zote zitakazozalishwa na mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma zisafirishwe kupitia bandari ya Mtwara.

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini, TPA, Juma Kijavara amesema jana Oktoba 4, 2023 katika kikao cha wadau wa usafirishaji wa korosho kupitia bandari ya Mtwara kuwa TPA imejiandaa vya kutosha kuhakikisha agizo hilo linatekelezeka.

Aidha mfanyabiashara na msafirishaji wa korosho, Omega Mnari amesema wafanyabiashara wamefurahia uamuzi huo wa serikali kwani kusafirisha korosho kupitia bandari ya Mtwara ni salama zaidi kwa upande wao.