Dk Mwigulu: Tozo ya miamala si michango ya kirafiki ni sheria ya Bunge

Dk Mwigulu: Tozo ya miamala si michango ya kirafiki ni sheria ya Bunge

Muktasari:

  • Waziri wa Fedha na Mipango nchini Tanzania, Dk Mwigulu Nchemba amesema  tozo za miamala ya simu si michango ya kirafiki ni sheria iliyopitishwa na  Bunge baada ya kujadiliwa kwa kina  akibainisha kuwa wabunge ni wawakilishi wa wananchi.



Dar es Salaam. Waziri wa Fedha na Mipango nchini Tanzania, Dk Mwigulu Nchemba amesema  tozo za miamala ya simu si michango ya kirafiki ni sheria iliyopitishwa na  Bunge baada ya kujadiliwa kwa kina  akibainisha kuwa wabunge ni wawakilishi wa wananchi.

Dk Nchemba amezungumza hayo leo Ijumaa Agosti 20, 2021 katika mkutano wake na waandishi wa habari akieleza kuwa fedha zilizopatikana baada ya ukusanyaji wa tozo tangu sheria ilipoanza kutumika mwezi mmoja uliopita,  zimetumika kuboresha sekta ya afya,  elimu na miundombinu.

 “Yaani inanyesha mvua moja tu mtoto inabidi alale shuleni hivi nani anaweza kumuamini jirani tu mtoto alale kila siku mto unapofungwa embu niambie mzazi unalala usingizi wa aina gani, kuna vitu ni serious kweli kweli ambavyo wabunge wanavisemea ambavyo vinatulazimisha tufunge mikanda, ”amesema Dk Mwigulu.


Amesema  nchi ndio zinavyojengwa hivyo amewapongeza watanzania wote ambao wanatoa mawazo mazuri ya kuboresha jambo hilo.

Leo Waziri huyo ameeleza kuwa katika kipindi cha wiki nne tangu kuanza kukata tozo ya miamala,   Serikali imekusanya Sh48.4 bilioni huku zaidi ya Sh22 bilioni zimepelekwa katika vituo vya afya.