Dk Mwinyi afurahishwa na wingi wa wapiga kura vituoni
Muktasari:
Mgombea urais Zanzibar kwa tiketi ya CCM, Dk Hussein Mwinyi amesema usalama upo wa kutosha, wapiga kura ni watulivu licha ya baadhi ya maeneo kuwa na mvua
Unguja. Mgombea urais Zanzibar kwa tiketi ya CCM, Dk Hussein Mwinyi, amefurahishwa na idadi kubwa ya wapiga kura iliyojitokeza katika vituo mbalimbali.
Amesema hayo leo baada ya kutembelea vituo mbalimbali vya kupigia kura mjini Unguja.
Dk Mwinyi amesema amefurahishwa na idadi kubwa ya wapiga kura vituoni na shughuli hiyo inavyoendeshwa kwa utulivu na hali ya ulinzi imeimarishwa.
Amewasisitiza wananchi kuendelea kujitokeza kupigia kura.
"Usalama upo wa kutosha, wapiga kura ni watulivu licha ya baadhi ya maeneo kuwa na mvua, lakini wametulia wanaendelea kutimiza haki yao ya kikatiba, niwaombe waliopo majumbani na kwingineko waendelee kujitokeza kutimiza haki yao ya msingi," amesema Dk Mwinyi.