Dk Mwinyi ataja changamoto kero za Muungano

Dk Mwinyi ataja changamoto kero za Muungano

Muktasari:

  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Mwinyi amesema licha ya kero nyingi za Muungano kupatiwa ufumbuzi lakini hazitakwisha kabisa kwasababu yapo mambo yanayoibuka kulingana na mahitaji na matakwa ya wakati uliopo.

Unguja. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Mwinyi amesema licha ya kero nyingi za Muungano kupatiwa ufumbuzi lakini hazitakwisha kabisa kwasababu yapo mambo yanayoibuka kulingana na mahitaji na matakwa ya wakati uliopo.

Dk Mwinyi ametoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na wahariri na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari kutoka Tanzania bara na Zanzibar Ikulu visiwani humo huku akitaja akaunti ya pamoja kuwa miongoni mwa changamoto kubwa zilizopo hivi sasa na ugumu wa kuipatia ufumbuzi.

Hata hivyo alisema katika kero zote zilizopo hivi sasa hakuna inayonyima usingizi.

“Changamoto nyingi zimeshafanyiwa kazi kwakweli mambo yanaenda vizuri tupo kwenye hatua nzuri zaidi, tumeshuhudia hata hivi karibuni zimeondoolewa karibu kero 11 zimebaki saba,” alisema na kuiongeza kuwa

“Lakini niseme tu kwamba changamoto za Muungano hazitafika mwisho kwahiyo matatizo yatakuwa yanaibuka lakini yanashughulikiwa,” alisema Dk Mwinyi

Alitolea mfano wa changamoto kubwa iliyopo hivi sasa kuwa ni akaunti ya pamoja ambayo fedha zote zinatakiwa ziingizwe kwenye akaunti hiyo kisha zitakuwa zinatolewa gharama za kuendesha nchi na fedha zinazobaki zinagawanywa.

Hata hivyo akaunti hiyo haijawahi kuundwa kwa kile Dk Mwinyi alichokiita kuwa kuna ugumu wake wa kuunda akaunti hiyo huku akisema tayari mchakato wake umeshaanza maana kila kitu kinamalizwa kwa mazungumzo.

“Kila jambo linazungumzika kwahiyo hata jambo hilo limeanza kuzungumzika imani yangu hili nalo litapata ufumbuzi maana tayari imeshaundwa kamisheni ya pamoja ya kulishghulikia watakaa na kuona namna bora ya kulimaliza.

Kinacholeta ugumu

Mfano Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ikikusanya kodi Zanzibar fedha hizo zinabaki huko kwa ajili ya matumizi ya Zanzibar, pia kuna Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) ambayo nayo inakusanya mapato lakini pia nayo yanabaki kuwa kwenye matumizi ya Zanzibar.

Pia alisema uendeshaji wa taasisi za Muungano kama Jehi la Polisi na Jeshi la Wananchi (JWTZ) uendeshaji wake, fedha zake zinatoka kwenye mfuko wa Seriklai ya Muungano lakini kukiwa na mfuko huo fedha hizo zitatakiwa zitoke kwenye mfuko wa pamoja.

Kuvunja baraza la Mawaziri

Akizungumzia utendaji usioridhisha wa baadhi ya viongozi Dk Mwinyi alisema ataendelea kufanya mabadiliko kila inapohitajika kwasababu ya utendaji kazi wao huku akisema hata baraza la mawaziri linaweza kufanyiwa marekebisho wakati wowote kutokana na utendaji kazi wao.

“Nimekaa serikalini miaka 20, sijawahi kuona baraza la Mawaziri linaanza mwanzo hadi mwisho kwahiyo kubaidlishwa kupo, anayefanya vizuri tutakwenda naye asiyefanya vizuri tutamuweka pembeni,”

Uwanja wa ndege kupewa mwekezaji wanje

Alisema Serikali imeamua kutafuta kampuni kubwa zenye sifa duniani kushiriki uendeshaji wa kiwanja cha ndege cha Amani Abeid Karume kwa lengo la kutoa huduma bora za kiwango cha kimataifa.

Alisema nia ya serikali ni kukifanya kiwanja hicho kiwe na sifa za akimataifa na kutoa huduma bora kwani wageni walikuwa wakipata kero kubwa wakati mwingine kukaa zaidi ya saa tatau wakikaguliwa.

Kwahiyo ni ni nzuri tunataka kuona mabadiliko katika uwanaj wetu

Hivi karibuni Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar (ZAA) na kampuni za kimataifa za Dnata, Eg's, Emirates na Segap ambayo inahusu kutoa huduma za abiria na mizigo, uendeshaji wa uwanja wa ndege, kumbi na maduka na migahawa vilivyomo ndani ya uwanja huo.

Usuli wa kero za muungano;

Mwaka 1964 mataifa mawili Tanganyika na Zanzibar yaliungana na kuitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya waasisi wake Julius Nyerere na Aman Abeid Karume.

Hata hivyo licha ya muungano huo kumekuwapo na masuala mbalimbali ambayo hulalamikiwa na kuitwa kero za muungano ambayo hulalalmikiwa na pande zote mbili.

Kutokana na hali hiyo, Serikali ya Jamhuri ya Muungano (SMT) na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), ziliweka utaratibu wa kutatua changamoto hizo kupitia mfumo rasmi wa vikao vya kamati ya pamoja ya SMT na SMZ ya kushughulikia masula ya mmungano.

Tangu kuanzishwa kwa utaratibu huo mwaka 2006, hoja 25 zilijadiliwa na hadi kufikia Oktoba 17, 2020 jumla ya hoja saba zilikuwa zimepatiwa ufumbuzi na kubaki 18 kabla ya zingine 11 kupata ufumbuzi Agosti 24, 2021.

Katika kikao kilichofanyika siku mbili Agosti 23 na 24, 2021 mjini Unguja jumla ya hoja 11 zilipatiwa ufumbuzi na tisa kati ya hizo zilisainiwa hati ya makubaliano ya kuziondoa na kubaki hoja saba ikiwemo mgawanyo wa mapato (akaunti ya pamoja.