Dk Mwinyi ateua viongozi wapya wizara ya afya

Rais wa Zanzibar,  Dk Hussein Mwinyi

Muktasari:

  • Rais wa Zanzibar Dk Hussein Mwinyi amefanya uteuzi mbalimbali akiwemo Mkemia Mkuu wa Serikali, Dk Farid Mzee Mpatani.

Unguja. Rais wa Zanzibar Dk Hussein Mwinyi amefanya uteuzi mbalimbali akiwemo Mkemia Mkuu wa Serikali, Dk Farid Mzee Mpatani.

Taarifa iliyotolewa na Ikulu na kusaniwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Zena Said, imesema uteuzi huo umeanza leo Ijumaa Septemba 23, 2022.

Kabla ya uteuzi huo, Dk Farid alikuwa ofisa Mkuu uchunguzi wa Maabara katika wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu Zanzibar.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wengine walioteuliwa ni Dk Salim Nassor Slim ambaye anakuwa Mkurugenzi Kinga na elimu ya afya. Kabla ya uteuzi huo, Dk Salim alikuwa Naibu Mkurugenzi wa idara hiyo.

Dk Msafiri Ladislaus Marijani ametuliwa kuwa mkurugenzi wa idara ya tiba. Kabla ya uteuzi huo Dk Msafiri alikuwa Mkurugenzi Mkuu Hospitali ya Mnazi Mmoja huku nafasi yake ikichukuliwa na Dk Muhidin Abdi Mahmoud ambaye alikuwa Daktari bingwa wa magonjwa ya figo hospitali ya Taifa Muhimbili.

Mwingine aliyeteuliwa ni Dk Fatma Mohamed Kabole mbaye anakuwa naibu Mkurugenzi kinga na elimu ya Afya, kabla ya uteuzi huo Dk Fatma alikuwa Mkuu wa kitengo cha maradhi yasiyopewa kipaumbele.

“Khamis Bilal Ali ameteuliwa kuwa Ofisa Mdhamini wizara ya Afya –Pemba, kabla ya uteuzi huo Khamis alikuwa Mkuu wa idara ya Kinga na Elimu ya Afya-Pemba,” imesema