Dk Mwinyi awateua Mazrui, Mkuya na Shaaban kuwa mawaziri

Muktasari:

  • Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi ameteua mawaziri watatu huku wawili wakiwa makada wa chama cha ACT-Wazalendo.

Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi ameteua mawaziri watatu huku wawili wakiwa makada wa chama cha ACT-W

Unguja. Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi ameteua mawaziri watatu huku wawili wakiwa makada wa chama cha ACT-Wazalendo.

Nassor Ahmed Mazrui ambaye ni naibu katibu mkuu wa ACT Zanzibar ameteuliwa kuwa waziri wa afya, ustawi wa jamii, jinsia, wazee na watoto.

Taarifa iliyotolewa leo Jumatano Machi 3, 2021 na katibu mkuu kiongozi Zanzibar, Zena Said inaeleza kuwa Omar Said Shaaban ambaye ni mwanasheria mkuu wa chama hicho, ameteuliwa kuwa waziri wa biashara na maendeleo ya viwanda.

Dk Mwinyi pia amemteua Dk Saada Mkuya kuwa waziri wa nchi, ofisi ya makam wa kwanza wa Rais Zanzibar.

Inaeleza kuwa Rais Mwinyi amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa vifungu vya 42, 43(1)(2) na 44 vya katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 na kwamba walioteuliwa wataapishwa kesho Alhamisi Machi 4, 2021 saa 4 asubuhi.

Katika hafla hiyo ya kuapisha, kiongozi huyo pia atamuapisha kamishna wa bodi ya mapato Zanzibar, Salum Yssuf Ali ambaye aliteuliwa Februari 10, 2021.