Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dk Mwinyi kuzindua Maonyesho ya Sabasaba

Muktasari:

  • Maonyesho ya Sabasaba yaliyohudhuriwa na nchi 23 yamekusanya kampuni zaidi ya 3,400 za ndani na nje ya nchi huku zikibeba fursa mbalimbali

Dar es Salaam.   Tofauti na miaka ya nyuma, Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) yalikuwa yakizinduliwa tarehe za mwanzo Julai, mwaka huu ni tofauti kwa kuwa, uzinduzi rasmi utafanyika siku ya kilele cha Sabasaba.

Huu ni mwendelezo wa upekee huku ndani yake ukifanyika uzinduzi wa nembo ya ‘Made in Tanzania’ inayotajwa kuwa kitambulisho muhimu cha bidhaa za Tanzania.

Hayo yamesemwa leo Julai 2, 2025 na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Selemani Jafo baada ya kukagua mabanda ndani ya Uwanja wa Julius Nyerere katika Maonyesho ya Sabasaba yanayoendelea jijini hapa.

Dk Jafo amesema maonyesho ya mwaka huu yatafunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi na kufungwa na Julai 13 mwaka huu na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

“Watanzania hii ni fursa ya kutangaza biashara zetu ziwe shindani, sisi Watanzania ni wanachama wa masoko mbalimbali ikiwamo Jumuiya ya Afrika ya Mashariki na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na kuna soko huru la Afrika lenye watu zaidi ya 1.4 bilioni,” amesema Dk Jafo.

 “Pia, maonyesho haya ni ya kimataifa na nchi mbalimbali zinakuja siku hizi kushiriki, hivyo ni fursa ambayo lazima tuitumie.”

Amesema maonyesho hayo yatachangia ukuzaji wa pato la Taifa huku akisema yale yanayoendelea kufanyika yatabadili zaidi ukuaji wa uchumi nchini.

Akizungumzia uzinduzi wa nembo ya ‘Made in Tanzania’ ambao utafanywa na Naibu Waziri Mkuu, Dk Doto Biteko  amesema ilikuwa ni mchakato wa muda mrefu na kampuni zaidi ya 90 zilishiriki hadi kupatikana moja.

Jafo amesema nembo hiyo inaenda kuweka alama katika eneo la biashara kwa kuwa, Tanzania imekuwa ikifanya vizuri katika uzalishaji lakini bidhaa zake hazitambuliki vizuri katika masoko ya nje.

Hiyo ni baada ya baadhi ya bidhaa zinazozalishwa nchini kuwa zaidi ya mahitaji yaliyopo jambo linalohitaji masoko zaidi.

“Kwa mfano, saruji mahitaji yetu ni tani milioni nane na sasa tunazalisha tani milioni 10, mahitaji ya sukari ni tani 802,000 lakini sasa inapanda, hadi mwaka 2027 tutakuwa tumejitosheleza, hivyo lazima kuwe na nembo ya Made in Tanzania,” amesema.

Pia, amesema uzalishaji wa bidhaa za kioo nazo zimeongezeka kiasi cha kuhitaji kupelekwa nje ya nchi kwa ajili ya kuuza, hivyo ni lazima iwepo nembo inayoitambulisha nchi.

Akizungumza mmoja wa wafanyabiashara wa bidhaa za viungo, Farhia Minja amesema uwepo wa nembo hiyo itawasaidia kufikia masoko ya nje kwa urahisi zaidi.

“Kwa sababu itakuwa ni ile inayotambulika kimataifa, tofauti na sasa kila mmoja anajiwekea ya kwake, hiki ni kitu ambacho tunaweza kusema kilichelewa lakini ni bora kimekuja,” amesema Farhia.