DPP asamehe wafungwa 183 Karagwe
Muktasari:
Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DDP), Biswalo Mganga amewafutia mashtaka mahabusu 183 katika magereza ya Karagwe, Bukoba, Biharamulo na Muleba mkoani Kagera.
Karagwe. Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DDP), Biswalo Mganga amewafutia mashtaka mahabusu 183 katika magereza ya Karagwe, Bukoba, Biharamulo na Muleba mkoani Kagera.
Amesema hayo leo Alhamisi Januari 21, 2021 katika ziara yake ya kikazi Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera.
Amesema baada ya kutembelea katika magereza hizo na kuzungumza na mahabusu amewafutia mashtaka mahabusu 57 wa Wilaya ya Karagwe, Bukoba 54, Biharamulo 48 na Muleba 26.
Amewataka wananchi kuishi nao vizuri wanaporejea uraiani ili kujenga jamii yenye amani, upendo na mshikamano.
Mganga amesema kuwa katika ziara yake hiyo ya kutembelea magereza alikuta wahamiaji haramu 15 waliokaribishw ana wananchi ambao ni wenyeji wa mkoa huu.
Jaji wa mahakama kuu Kanda ya Kagera, Ntemi Kilekamajenga
amesema Mkoa wa Kagera unaongoza kwa kuwa na kesi nyingi za mauaji na kuwaomba viongozi wa dini kuhubiri amani.
Amesema kesi nyingi zingeweza kumalizwa kwa njia ya usuluhishi nje ya mahakama hivyo kuipunguzia Serikali gharama za uendeshaji wa kesi.
Jaji Kilekamajenga amesema katika mkoa wa Kagera kesi ambazo zipo katika hatua ya kusikilizwa zinakaribia kuvuka 450 hivyo mkoa wa Kagera unaweza kuwa wa pili au watatu kwa Tanzania kuwa na kesi nyingi za mauaji.
Katika hatua nyingine amezindua ofisi ya mwendesha mashtaka Wilaya ya Karagwe ili kuwapunguzia gharama wananchi na kupunguza ucheleweshaji wa mashauri mahakaman