Fahamu magonjwa yaliyomuua Lowassa

Muktasari:

  • Tanzania ipo kwenye simanzi baada ya kumpoteza aliyekuwa Waziri mkuu, Edward Lowasa kufariki dunia wakati akiendelea na matibu katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).

Dar es Salaam. Miongoni mwa taarifa zilizoibua simanzi mchana wa leo ni kifo cha Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, ambaye ameugua kwa takribani miaka miwili.

 Lowassa amefariki leo Februari 10, 2024 saa nane mchana katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ya jijini Dar es Salaam, huku jambo ambalo wengi wanatamani kujua  kiongozi huyo alikuwa anaumwa ugonjwa gani.

Kwa mujibu wa Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango,  Lowassa aliyekuwa na miaka 70, alikuwa akipatiwa matibabu ya magonjwa ya kujikunja utumbo, matatizo ya mapafu na shinikizo la damu.

“Hayati Lowasaa ameugua muda mrefu na amekuwa akipatiwa matibabu tangu tarehe 14, Januari 2022 katika taasisi ya moyo ya Jakaya kikwete na baadaye akapelekwe kwa matibabu zaidi Afrika kusini na baadaye kurejea,” amesema Dk Mpango wakati akitangaza msiba wa Lowassa.

Akiwa nchini humo kwa matibabu Lowassa alitembelewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Desemba 28, 2022 na kuwasilisha salamu za Rais, Samia Suluhu Hassan.


Endelea kufuatilia Mwananchi na mitandao yetu kwa habari zaidi.