FOCAC ni msukumo wa maendeleo endelevu ya ushirikiano kati ya China na Tanzania

Thursday December 03 2020
New Content Item (1)

Mhe. Wang Ke, Balozi wa China nchini Tanzania

Mwaka huu ni kumbukumbu ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Mwanzoni mwa karne ya 21, kuendana na hali mpya, kutumia fursa mpya na kukabiliana na changamoto mpya, China na Afrika kwa pamoja zilipendekeza kuanzishwa kwa FOCAC, ambayo imeingiza uhusiano wa China na Afrika katika enzi mpya iliyo na maendeleo yaliyounganishwa na ya kitaasisi.

Tangu wakati huo, ushirikiano wa China na Afrika umekwenda kwenye “gia ya juu”, ikiendelea kwenye “njia ya haraka”. Katika kipindi cha miaka 20 iliyopita, FOCAC imekuwa ikitanuka na kuendelea kila wakati. Imekuwa jukwaa muhimu la mazungumzo ya pamoja na utaratibu mzuri wa ushirikiano wa kiutendaji kati ya China na Afrika.

Pia imekuwa bendera ya ushirikiano wa Kusini na Kusini na ushirikiano wa kimataifa na Afrika. Jukwaa limetoa nafasi kwa uhusiano kati ya China na Afrika kutoka “aina mpya ya ushirikiano” hadi “aina mpya ya ushirikiano wa kimkakati” na “ushirikiano kamili wa kimkakati na ushirika”, na kuimarisha imani ya kimkakati kati ya China na Afrika kufikia kiwango cha juu.

FOCAC haijawahi kuwa “Jukwaa la mazungumzo”, bali “kikosi kazi” ambacho hufanya mambo yatendeke. Katika kipindi cha miaka 20 iliyopita, FOCAC imeunda na kutekeleza safu ya hatua zinazolenga matokeo, mipango na hatua zinazokidhi mahitaji ya China na Afrika, na kuleta faida zinazoonekana kwa Wachina na Waafrika.


Mwaka 2019, uwekezaji wa moja kwa moja we Wachina barani Afrika ulikuwa Dola za Marekani bilioni 49.1, ikiongezeka kwa karibu mara 100 kutoka mwaka 2000; Biashara ya China na Afrika ilifikia Dola za Marekani bilioni 208.7, ikiwa ni mara 20 kwa ukubwa wa mwaka 2000.

Advertisement

China imekuwa mshirika mkubwa wa kibiashara barani Afrika kwa miaka 11 mfululizo, na imechangia zaidi ya 20% ya ukuaji wa Afrika kwa miaka kadhaa. Miradi mingi ya kimkakati, kama Kituo cha Mikutano cha Umoja wa Afrika (AU), Reli ya Addis Ababa-Djibouti, na Reli ya MombasaNairobi, imekamilika na kutumika. Miradi mingi ikiwa ni pamoja na reli, barabara, viwanja vya ndege, bandari za baharini na vituo vya umeme vimeanza kuzaa matunda barani Afrika.

Kufikia sasa, China imetoa takriban udhamini wa masomo wa serikali 120,000 kwa Afrika, na ilituma madaktari na wauguzi 21,000 katika timu za matibabu kwa mataifa 48 ya Afrika.

Takwimu na mifano hii ni maelezo wazi ya kujitolea kwa China na Afrika kukuza maendeleo ya pamoja, na ushahidi thabiti wa faida ya pande zote na hali ya umoja wa ushirikiano kati ya China na Afrika.

Ikumbukwe kwamba FOCAC imeuonyesha ulimwengu nguvu ya uhusiano wa China na Afrika unaojulikana na mshikamano, usaidizi wa pande zote, mashauriano mapana na mchango wa pamoja. Imeonyesha pia uwezo mkubwa wa maendeleo ya Afrika, na kuongeza sura na hadhi ya kimataifa ya Afrika.


Mwaka 2000, Afrika iliitwa “Bara lisilo na Tumaini” katika jarida maarufu la The Economist, ambalo liliwakilisha maoni ya jumla ya Afrika katika ulimwengu wa Magharibi. Walakini, wakati wa miaka 20 baada ya kuanzishwa kwa FOCAC, uchumi wa Afrika umeonyesha kwa ulimwengu kasi ya ukuaji wa kusisimua, na Afrika imechukua sura mpya iliyo na amani ya kudumu na maendeleo endelevu.

Hivi sasa, Afrika inachukuliwa kama “Bara lenye Tumaini” na mahali pazuri kwa uwekezaji, na njia mbalimbali za kimataifa za ushirikiano na Afrika zimeanzishwa. Ni sawa kusema kwamba FOCAC haijaleta tu mabadiliko ya kushangaza katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya Afrika, lakini iliongoza na kukuza ushirikiano wa kimataifa na Afrika, na hivyo kuchangia pakubwa katika namna mbalimbali za washirika wa ushirikiano wa Afrika.

Kama nchi muhimu barani Afrika na mshirika wa ushirikiano wa jadi wa China, Tanzania imekuwa na jukumu muhimu katika uanzishaji na maendeleo ya FOCAC. Mnamo Oktoba 2000, wakati Rais wa Tanzania wakati huo Benjamin Mkapa alikuwa katika kipindi chake muhimu cha kampeni za kuchaguliwa tena, alichukua uamuzi wa kwenda China kuhudhuria Mkutano wa Kwanza wa Mawaziri wa FOCAC, na hivyo kuwa mmoja wa viongozi wanne wa Afrika walioshuhudia kuanzishwa kwa FOCAC.


Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania Dk. Salim Ahmed Salim, Katibu Mkuu wa Umoja wa Afrika wakati huo (OAU), pia alikuwepo kwenye mkutano huo. Katika miaka 20 iliyofuata, Tanzania ilishiriki katika mikutano yote, makongamano ya mawaziri, mikutano ya waratibu, mikutano ya maafisa wakuu na vikao vikuu katika mfumo wa FOCAC, ikichangia kikamilifu hekima na nguvu zake kwa maendeleo ya Jukwaa.

Mnamo mwaka 2018, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akimwakilisha Rais John Pombe Magufuli, alihudhuria Mkutano wa FOCAC Beijing, na alikutana na Rais wa China Xi Jin-ping. Viongozi hao wawili walifanya majadiliano ya kina juu ya maendeleo ya uhusiano kati ya China na Tanzania.

Katika kipindi cha miaka 20, China na Tanzania zimedumisha mawasiliano ya kimkakati na kuimarisha ushirikiano wa faida kati ya mfumo wa FOCAC. Nchi hizi mbili zimefanya juhudi za pamoja kutekeleza matokeo ya kila mkutano wa Jukwaa na hivyo kuendelea kutoa msukumo mpya kwa ushirikiano wa ushindi kwa pande zote na maendeleo ya pamoja ya China na Tanzania.

----Biashara na uwekezaji wa nchi mbili umefikia kiwango kipya. Mnamo mwaka wa 2019, biashara ya China na Tanzania ilifikia Dola za Kimarekani bilioni 4.179, ikiwa ni mara 45 ya ukubwa wa mwaka 2000. China imekuwa mshirika mkubwa wa kibiashara wa Tanzania kwa miaka minne mfululizo.


Uwekezaji jumla wa moja kwa moja wa China nchini Tanzania umezidi dola za Kimarekani bilioni 7, na miradi zaidi ya 700 ya uwekezaji ikitoa karibu ajira 150,000 za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja kwa Watanzania. Biashara za Wachina zimeanzisha ustawi katika sekta kama vile mavazi, usindikaji wa bidhaa za kilimo na utengenezaji wa vifaa vya ujenzi.

Uwekezaji huu umechangia utekelezaji wa mkakati wa kuhimiza vitu vya ndani wa Tanzania katika maende-leo ya uchumi na mchakato wake wa viwanda pia.

---Alama nyingi angavu zimejitokeza nchini Tanzania. Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) ni jengo lingine la kumbukumbu linaloashiria urafiki kati ya China na Tanzania kufuatia Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA).

Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ni maktaba kubwa na ya kisasa zaidi iliyojengwa kwa msaada wa Wachina barani Afrika. Miongoni mwa miradi ya miundombinu inayofanywa na kampuni za Wachina, Daraja la Nyerere ni daraja la kwanza la kuvuka bahari katika Afrika Mashariki; Barabara ya juu ya Ubungo ndio njia ya kwanza ya safu nyingi na mbalimbali nchini Tanzania; na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano (NICTBB) ni “Njia Kuu ya Habari” ya Tanzania ambayo inashughulikia nchi nzima na inaunganisha mataifa jirani.

----Ushirikiano wa kuboresha maisha ya watu umetoa mafanikio ya ajabu. Katika kipindi cha miaka 20, China imetuma timu 22 za matibabu zilizojumuisha madaktari 490 kwenda Tanzania Bara na Zanzibar.

Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), iliyojengwa kwa msaada wa China, imefanya upelekaji wa wagonjwa kwenda nchi za nje kwa upasuaji wa moyo kuwa jambo lililopita. China imetoa ufadhili wa serikali kwa wanafunzi wa Kitanzania 2,339 na karibu fursa 7,000 za mafunzo ya muda mfupi kwa wataalamu mbalimbali wa Kitanzania katika kipindi cha miaka 20 iliyopita. China pia imefadhili ujenzi wa Kituo cha Mafunzo ya Ufundi na Huduma ya Mkoa wa Kagera, na upanuzi wa Chuo ya Polisi ya Tanzania Moshi, kwa madhumuni ya kuunga mkono juhudi za Tanzania kukuza nguvu kazi.

--- Mabadilishano ya WatukwaWatu yamekuwa yakistawi. Miaka ya hivi karibuni imeshuhudia kuongezeka kwa idadi ya vijana wa Kitanzania kwenda China kusoma au kufanya kazi. Wakati huo huo, Wachina zaidi na zaidi wanavutiwa na Tanzania kwa biashara, masomo ya elimu, uwekezaji na utalii.

“Sikukuu njema ya Mwaka mpya wa Jadi -Kusherekea Mwaka Mpya wa Kichina nchini Tanzania”, Mashindano ya Kimataifa ya Wushu (Sanaa ya Vita) na shughuli nyingine za kitamaduni za Wachina zimekuwa chapa maarufu za mabadilishano ya kiutamaduni kati ya China na Tanzania. Tinga Tinga na sanaa zingine za kipekee za zinazotengenezwa Tanzania zimevutia mashabiki wengi nchini China.

Kwa kuongezea, idadi ya watalii wa China waliotembelea Tanzania mnamo 2019 ilizidi 35,000, na safari za moja kwa moja kati ya Dar es Salaam na Guangzhou ziko kwenye maandalizi. Wiki chache zilizopita, mkutano wa 5 wa Kamati Kuu ya 19 ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ulipitisha mapendekezo ya Kamati Kuu ya CPC ya kuunda Mpango wa 14 wa Miaka Mitano (2021-2015) wa Maendeleo ya Uchumi ya kitaifa na kijamii na Malengo kwa kipindi cha mwaka wa 2035. Mapendekezo haya yanaonyesha mwongozo mkuu wa maendeleo ya baadaye ya China.

Kukamilika kwa Uchaguzi Mkuu wa sita na kuchukua majukumu ya viongozi wa kitaifa na Bunge, Tanzania inaenda kwa kasi kubwa kufikia utimilifu kamili wa malengo yaliyowekwa katika Dira yake ya Maendeleo ya 2025.

Kama China na Tanzania zimeingia katika kipindi kipya cha maendeleo, nchi hizo mbili zinakabiliwa na fursa za kuimarisha mshikamano na ushirikiano kwa manufaa ya wote.

China inategemea kupanga mikakati ya maendeleo na kuimarisha mawasiliano ya sera, na kuharakisha utekelezaji wa matokeo ya Mkutano wa FOCAC Beijing na Mpango wa Ukanda na Njia Moja, Kwa kutumia kikamilifu rasilimali na majukwaa ya FOCAC, tunaweza kukuza maendeleo ya nchi mbili na kufanya uhusiano kati ya China na Tanzania kuwa mfano mzuri wa kujenga jamii ya karibu ya China-Afrika na maisha yenye mustakabali kwa wote.

Advertisement