Gavana BOT ataja sarafu zinazotumika Tanzania

Sunday June 13 2021
sarafu pic
By Mgongo Kaitira

Mwanza. Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Profesa 

Florens Luoga ametaja sarafu ambazo zipo katika matumizi nchini.

Akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa jengo la benki hiyo Mkoa wa ,  Profesa Luoga amesema pamoja na BoT kusisitiza uzalishaji wa baadhi ya sarafu, bado kuna sarafu zinaendelea kutumika hasa  mtu anapolipa kodi au bili mbalimbali.

Amesema sarafu ambazo pamoja na BoT kusitisha uzalishaji na usambazaji wake lakini zinaendelea kutumika kuwa ni senti tano, senti ishiriki,  shilingi moja, shilingi tano, 10 na 20.

Amezitaja sarafu ambazo zinaendelea kuzalishwa na kusambazwa katika shughuli za kifedha kuwa ni Sh50, Sh100, Sh200 na Sh500.

Amewataka wananchi kuendelea kutambua matumizi ya sarafu hizo wakati wowote wanapofanya miamala yao ya kifedha.

Advertisement


Advertisement