Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hali ngumu jijini Nairobi mafuta yakipanda bei

Muktasari:

  • DW Swahili imeripoti kuwa tangazo hilo linatimiza kigezo cha Shirika la Fedha Duniani (IMF), inayoishinikiza Kenya kusitisha mpango wa kutoa ruzuku kwa bidhaa za petroli ifikapo Oktoba mwaka huu.

Dar es Salaam. Bei ya mafuta na petroli nchini Kenya imepanda kwa KSh20 zikiwa ni siku mbili tangu Rais William Ruto kutangaza kuwa ruzuku kwenye bidhaa za petroli itaondolewa.

DW Swahili imeripoti kuwa tangazo hilo linatimiza kigezo cha Shirika la Fedha Duniani (IMF), inayoishinikiza Kenya kusitisha mpango wa kutoa ruzuku kwa bidhaa za petroli ifikapo Oktoba mwaka huu.

Siku mbili baada ya Rais Ruto kutangaza kuwa bei ya mbolea itashushwa kwa nusu, bei ya mafuta na petroli imepanda kwa KSh20 hii leo.

Haya yanajiri wakati ambapo Kenya inajitahidi kutimiza masharti IMF, ulioipa Serikali mkopo wakati wa utawala wa Rais Uhuru Kenyatta.

IMF inajumuisha nchi 188, na lengo lake kuu la kuanzishwa kwake ni kuleta utulivu wa kifedha duniani.

Kwa sasa lita moja ya petroli itauzwa kwa KSh179 kutokea KSh159, bei ambayo ni sawa na ongezeko la KSh20.

Bei ya mafuta ya dizeli imeongezeka kwa KSh25, na hivyo kufanya lita moja ya mafuta hayo kuuzwa jijini Nairobi, kwa KSh165.

Kwa upande wa mafuta ya taa, pia kunaongezeko la KSh20, ambapo sasa lita moja ya mafuta ya taa itauzwa kwa KSh147.94.

Bei zote hizo ni kwa jiji la Nairobi na kwamba zinajumulisha kodi ya ongezeko la thamani.

Bei hizo mpya zinaanza kutumika mara moja na zinaashiria kuwa ruzuku kwa bidhaa za petroli imefutiliwa mbali na kwa dizeli na mafuta ya taa imepunguzwa.

Mpaka sasa, Kenya imeshatumia dola bilioni 1.2 ambayo ni sawa na asilimia 86 ya pato lake la utalii kwa mwaka huu, kwa ajili ya kugharamia ruzuku yamafuta, hi ini kwa mujibu wa takwimu rasmi za Serikali.

Duru za uchumi zinaonyesha kuwa oOngezeko hilo la bei huenda likaathiri shughuli za kilimo na kuongeza gharama zake, hata hivyo; mwanzoni wa wiki hii, bei ya mbolea ilishushwa na wiki ijayo, ndiyo bei hiyo itaanza kutumika.

Wakulima wa maeneo ya kaskazini mwa bonde la ufa wanaojikita kwenye kilimo cha mahindi wana mtazamo hasi katika hili na hasa ukizingatia ulinganifu wa bei ya mbolea na pembejeo na hali halisi ya maisha ya wakulima hao.

Kwa upande mwengine, bei ya umeme nayo pia imeongezeka kwa asilimia 15.7; Ongezeko hilo linabatilisha punguzo lililotangazwa mwanzoni mwa mwaka huu na Rais aliyeondoka madarakani Uhuru Kenyatta.

Kwa mantiki hiyo, wateja wanaotumia zaidi ya ‘unit’ 100 za umeme majumbani mwao kwa mwezi, watalipa zaidi. Huku viwanda na makampuni makubwa, wakikabiliwa na bei kubwa zaidi za umeme kwani gharama za kusambaza nishati hiyo, zimeongezeka kwa zaidi ya theluthi moja.