Halmashauri 89 zakabiliwa na upungufu wa chakula

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka 2023/2024 leo Mei 8, 2023 bungeni jijini Dodoma. Picha na Merciful Munuo

Muktasari:

  • Upungufu wa uzalishaji katika baadhi ya maeneo kwa msimu wa 2021/2022 uliotokana na athari za mabadiliko ya tabia nchi, umesababisha kupanda bei kwa baadhi ya mazao ya chakula.

Dar es Salaam. Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) imesambaza tani 75,282.302 za chakula katika halmashauri 89 zenye upungufu wa chakula nchini.

 Hayo yamesemwa na Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe ameyasema hayo leo Jumatatu Mei 8, 2023 wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka 2023/2024.

Amesema tathmini ya kina ya hali ya chakula na lishe imebaini kuwa na upungufu wa uzalishaji katika baadhi ya maeneo kwa msimu wa 2021/2022 uliotokana na athari za mabadiliko ya tabia nchi na hivyo kusababisha kupanda bei kwa baadhi ya mazao ya chakula.

“Ili kukabiliana na hali hiyo, Wizara kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula imesambaza tani 75,282.302 za chakula katika Halmashauri 89 zenye upungufu wa chakula,”amesema.

Amesema chakula hicho kiliuzwa kwa bei kati ya Sh680 milioni hadi Sh 920 kwa kilo ikilinganishwa na bei ya soko ya Sh 1,200 hadi Sh1, 500.