Halmashauri Moshi yapiga marufuku mbege kuuzwa baa

Friday March 05 2021
New Content Item (2)

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Moshi, Moris Makoi

By Fina Lyimo

Moshi. Halmashauri ya Wilaya ya Moshi imepiga marufuku baa zinazouza mbege kufunguliwa pamoja na kupika chakula kwenye misiba.

Katazo hilo limetolewa  leo Ijumaa Machi 5, 2021 na mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Moris Makoi akibainisha kuwa lengo ni kupunguza maambukizi ya magonjwa ya mfumo wa hewa.

New Content Item (2)

Amesema watu husafiri kutoka mikoa mbalimbali na kuingia Moshi kwa ajili ya kushiriki mazishi na kusababisha msongamano, hasa wakati wa kula.

"Tumeshirikiana na viongozi wa dini pamoja na halmashauri ili kudhibiti hali hiyo kutokana na kuwepo kwa maambukizi ya magonjwa  mbalimbali,”

amesema Makoi

Advertisement

Amesema halmashauri  hiyo ina vitongoji 700 na vijiji 157 akibainisha kuwa kata ya Okaoni ina vitongoji 22 na kila kitongoji kina vilabu vya pombe kati ya sita hadi saba hali inayosababisha vijana wengi kuwa walevi.

Mkazi wa kijiji cha Kitandu, Bernad Massawe amesema ni vyema Serikali ikachukua hatua kuondoa vilabu vya pombe vilivyoibuka katika kijiji hicho kwa kuwa vijana wanaangamia kwa kunywa pombe kupita kiasi.

Advertisement