Haya hapa majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha tano, vyuo vya kati

Dar es Salaam. Wahitimu 188,787 kati ya 197,426 waliofaulu mitihani ya kidato cha nne, wamechaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha tano pamoja na vyuo mbalimbali kwa mwaka 2024.

Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Tawala za Miko ana Serikali za Mitaa (Tamisemi) Mohamed Mchengerwa amesema hayo leo Alhamisi Mei 30, 2024 wakati akitangaza uchaguzi wa wanafunzi.