Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hii ndio tamthiliya kamili ya Jacob Zuma kisiasa

Jacob Zuma

Muktasari:

  • Kifungo chake chachochea vurugu, polisi wakisema uhalifu umejipenyeza
  • Afrika Kusini inaandika historia. Dunia imezoea kushuhudia maandamano ya raia dhidi ya Serikali. Hukumu dhidi ya Rais wa tatu wa kidemokrasia, Jacob Zuma, ya kifungo cha miezi 15 jela, imeamsha hasira za umma.

     






Afrika Kusini inaandika historia. Dunia imezoea kushuhudia maandamano ya raia dhidi ya Serikali. Hukumu dhidi ya Rais wa tatu wa kidemokrasia, Jacob Zuma, ya kifungo cha miezi 15 jela, imeamsha hasira za umma.

Kosa la Zuma ni kudharau mahakama. Alipuuza wito wa kwenda mahakamani ili kutoa ushahidi wa kesi dhidi yake. Mashtaka ya Zuma yanahusu vitendo vya rushwa kipindi akiwa Rais. Aliiongoza Afrika Kusini kuanzia Mei 9, 2009 mpaka Februari 14, 2018.

Uamuzi wa mahakama kumfunga Zuma, umesababisha ghasia. Wanaomtetea, wapo mitaani. Mpaka jana vifo vilivyoripotiwa ni 78, huku watu zaidi ya 1,800 wakiwa wameshakamatwa na kutupwa mahabusu. Uharibifu wa mali ni mkubwa. Maduka makubwa, majumba, magari na mali nyingine zimekuwa zikichomwa moto.

Kituo kikubwa cha ununuzi (shopping mall), kwenye Jiji la Pietermaritzburg, KwaZulu-Natal, nyumbani kwa Zuma, kiliteketezwa kwa moto, yote hayo yanafanyika ili kufikisha kwa umma hasira zao. Uvamizi wa maduka na uporaji pia ni mkubwa. Polisi wanasema kuwa wahalifu wamejipenyeza kwenye makundi ya waandamaji.

Jacob Zuma,

Tuhuma za rushwa kwa Zuma zilikuwa za muda mrefu. Kwa miaka miwili mfululizo, kuanzia mwaka 2016 mpaka 2018, chama chake, ANC (African National Congress), kilimkingia kifua, kipindi ambacho wapinzani walishinikiza ang’oke madarakani. Hata hivyo, ilipofika Febuari 13, 2018, ANC ilitoa taarifa kuwa ilishamtaka Zuma aachie uongozi wa nchi na chama, lakini aligoma.

Februari 14, ndipo umma wa Waafrika Kusini ulipokea taarifa ya kiongozi wao, Zuma, aliyeongoza taifa hilo kwa miaka minane na ushehe, anaachia ngazi. Akaingia Rais Cyril Ramaphosa.

Kiini cha tatizo

Mwaka 2000, Benki ya Dunia ilianza kutumia msemo “State Capture”, ukiwa na maana ya mtu au kikundi cha watu kupenyeza ushawishi serikalini, matokeo yake Serikali inakuwa inafanya uamuzi wenye kunufaisha watu wachache kwa mazingira ya rushwa.

Msingi wa kesi ya Zuma ni “State Capture”. Zuma anatuhumiwa kuwa urafiki wenye mazingira ya rushwa na memba wa koo tajiri Afrika Kusini -- Gupta Family. Kwamba kipindi akiwa madarakani, familia ya Gupta ilikuwa na nguvu ya kuamua chochote kwenye nchi, ikiwemo hata kugawa vyeo.

Aliyekuwa mbunge Afrika Kusini kwa tiketi ya ANC, Vytjie Mentor, alipata kutoa ushuhuda kuwa aliwahi kuahidiwa uwaziri wa Biashara za Umma, kwa makubaliano kwamba baada ya kuwa waziri wa wizara hiyo, angesitisha safari za ndege za Shirika la Ndege Afrika Kusini kwenda India ili kutoa nafasi kwa Shirika la Jet Airways, kujitanua kibiashara kwenye njia hiyo ya India.

Jet Aways ni shirika ambalo Gupta Family wana ubia nalo. Mentor alisema, aliahidiwa uwaziri kwenye nyumba ya Gupta, Saxonwold, Johannesburg, kwamba siku alipopewa ahadi hiyo, Zuma naye alikuwa kwenye nyumba hiyo, ingawa vyumba tofauti. Familia ya Gupta, ilikanusha tuhuma hizo za ahadi hiyo wala kufanyika kwa kikao hicho.

Mentor alisema, yeye alikataa ofa ya uwaziri kutoka familia ya Gupta. Akaeleza kuwa siku chache baada ya kuzungumza na mwanafamilia ya Gupta, aliyekuwa Waziri wa Biashara za Umma, Barbara Hogan, aliondolewa kwenye nafasi hiyo na kuteuliwa mwingine.

Aliyekuwa Naibu Waziri wa Fedha Afrika Kusini, Mcebisi Jonas, naye alitoa ushuhuda kwamba mwaka 2015, aliitwa na watu wa familia ya Gupta, Saxonwold, Johannesburg. Baada ya kuitikia wito, aliahidiwa uwaziri wa fedha. Yaani Gupta Family walimuahidi kumpandisha cheo kutoka unaibu hadi uwaziri kamili wa fedha.

Tofauti na Mentor aliyesema alitakiwa kuzuia ndege za Afrika Kusini kwenda India, Jonas hakusema nini ambacho familia ya Gupta ilitaka awanfanyie baada ya kumpa uwaziri. Badala yake, Jonas alisema, yeye alikataa ‘ofa’ hiyo, kwa hoja kwamba hakuna mwenye ubavu wa kuteua waziri, isipokuwa Rais. Hata hivyo, Jonas alisema, siku chache baada ya kikao na familia ya Gupta, aliyekuwa Waziri wa Fedha, Nhlanhla Nene aliondolewa, kisha nafasi yake ikajazwa na Tito Mboweni.

Mwaka 2016, mwanaharakati Paul O’Sullivan, kupitia taasisi yake ya “Forensic for Justice”, alitoa ripoti yenye kuonyesha kuwa mfumo wa kukabiliana na jinai Afrika Kusini, uliwekwa mfukoni na watu. Forensic for Justice, imejikita katika mapambano dhidi ya uhalifu wa rushwa.

Kutokana tuhuma nyingi kwamba familia ya Gupta ilikuwa imeiweka serikali ya Zuma mfukoni, Machi 2016, padri wa Kanisa Katoliki, Stanslaus Muyebe aliwasilisha malalamiko ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Umma, Thuli Madonsela nakufungua faili la uchunguzi.Oktoba 14, 2016, ilikuwa siku ya mwisho Madonsela kuwa ofisini kama Mwendesha Mashtaka wa Umma, hivyo akapanga kuaga kwa kuachia ripoti ya uchunguzi kuhusu jinsi Gupta Family ilivyoiweka Serikali kiganjani. Zuma aliwasilisha ombi mahakamani kupinga na Mahakama ilipotupilia mbali ombi hilo, ripoti ikatoka Novemba 2, 2016 kila kitu kikawa hadharani. Zuma aliponda kuwa hakupewa nafasi ya kujitetea.

Kashfa nyingine

Katika kashfa ya ufisadi wa dili la Silaha Afrika Kusini, miaka ya 1990, Zuma pia alitajwa. Kashfa hiyo iliwahusisha pia mfanyabiashara tajiri Afrika Kusini ambaye alikuwa pia mshauri wa kifedha wa Zuma, Schabir Shaik pamoja na mdogo wake, Chippy Shaik. Kipindi hicho Zuma alikuwa makamu wa Rais.

Mwanasiasa na mfanyabiashara na Fana Hlongwane, alihusishwa kutokana na kuwahi kuwa mshauri wa kifedha wa aliyekuwa Waziri wa Ulinzi, enzi za utawala wa Mandela, Joe Modise, aliyefariki dunia mwaka 2001.

Wakati kashfa hiyo inaibuka mwaka 2002 na kutikisa Bunge mwaka 2003, Modise alikuwa ameshafariki dunia, hivyo akapona kutajwa lakini watu kadhaa walitajwa.

Mwaka 2003, aliyekuwa Mnadhimu wa ANC bungeni, Tony Yengeni alikiri kupokea rushwa, hivyo kufikishwa mahakamani na kuhukumiwa kifungo cha miaka minne jela mwaka 2004.

Kutokana na kashfa ya Dili la Silaha, Zuma aliondolewa kazini baada ya Shaik ambaye alikuwa mshauri wake wa kifedha, kukutwa na hatia kwenye ufisadi wa dili la silaha, hivyo kuhukumiwa kifungo jela miaka 15. Katika hukumu ya Shaik, jaji aliyeendesha kesi hiyo, Hilary Squires, alitaja jina la Zuma mara 471.