Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hitilafu ya umeme yaikwamisha treni ya SGR, huduma zarejea

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), safari za treni zilizothiriwa ni kutoka Dar es Salaam, Dodoma na Morogoro kwenda Dar es Salaam.

Dar es Salaam. Hitilafu iliyojitokeza katika mfumo wa Gridi ya Taifa, imesababisha kusimama gafla kwa treni ya mwendokasi iliyokuwa safarini Dar es Salaam, Morogoro na Dodoma, Shirika la Reli Tanzania (TRC) limeeleza.

Changamoto kwenye Gridi ya Taifa imejitokeza leo Jumatano, Desemba 4, 2024 na kuthibitishwa na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).

Hata hivyo, Tanesco imeeleza tayari hatua zimeshachuliwa na baadhi ya maeneo yaliyoathirika umeme umeanza kurejea, ikiwemo eneo la reli ya kisasa (SGR).

Taarifa ya abiria kukwama kwa muda kwenye SGR, imetolewa na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano TRC, Fredy Mwanjala leo, Desemba 4, 2024.

"Abiria walioathirika kufuatia hitilafu hiyo ya umeme ni wale walioanza safari yao saa 2:00 asubuhi kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma, abiria wa treni ya saa 3:30 asubuhi kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma na abiria waliotoka na treni ya saa 3:50 asubuhi kutoka Morogoro kwenda Dar es Salaam," imeeleza taarifa hiyo.

TRC imesema kutokana na jitihada zilizofanyika, umeme ulirejea saa 5:30 asubuhi na safari kurejea kama kawaida, hivyo inawaomba radhi abiria kwa usumbufu uliojitokeza.

Kupitia taarifa kwa umma iliyotolewa leo na Tanesco, imeeleza wataalamu wa shirika hilo wanaendelea na uchunguzi kubaini kiini cha tatizo hilo.

Tanesco imesema baadhi ya mikoa imeanza kupata huduma ya umeme. Mikoa iliyoanza kupata nishati hiyo ni Iringa, Dodoma, Morogoro na baadhi ya maeneo ya Dar es Salaam, Zanzibar na eneo la mradi wa SGR.

"Shirika linawaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza na litaendelea kutoa taarifa za hali ya urejeshaji wa huduma ya umeme kwa kadri hali inavyoimarika," imeeleza taarifa ya Tanesco.

Tatizo la umeme limetokea katika mikoa yote iliyounganishwa kwenye Gridi ya Taifa isipokuwa mikoa ya Lindi, Mtwara, Rukwa, Kigoma na Katavi ambayo haipo kwenye Gridi ya Taifa.