Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Huzuni yatawala Uwanja wa Jamhuri Dodoma

Huzuni yatawala Uwanja wa Uhuru

Muktasari:

  • Kifo hakizoeleki, kinaumiza ila ni mapezi ya Mungu. Ndivyo unavyoweza kusema kutokana na Janeth, mjane wa aliyekuwa Rais wa Tanzania, HayatI John Magufuli kushindwa kuvumilia na kuangua kilio wakati mwili wa kiongozi huyo ulipowasili katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Dar es Salaam. Kifo hakizoeleki, kinaumiza ila ni mapezi ya Mungu. Ndivyo unavyoweza kusema kutokana na Janeth, mjane wa aliyekuwa Rais wa Tanzania, HayatI John Magufuli kushindwa kuvumilia na kuangua kilio wakati mwili wa kiongozi huyo ulipowasili katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Mama Janeth alionyesha kuzidiwa na uchungu na kukaa chini, kiasi cha kushindwa kusimama tena wakati wimbo wa Taifa ukipigwa.

Sambamba na Mama Janeth, Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan pia alionekana kufuta machozi mara kwa mara.

Kwa takribani dakika 10,  Janeth alikuwa akilia kiasi cha kuwapa uchungu walinzi wake ambao licha ya kumtuliza na wao walionekana wakifuta machozi kwa uchungu.

Rais Samia licha ya kufuta machozi alionekana akimtuliza Janeth kwa kumshika mkono.