Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Idadi ya vifo ajali ya Chemba yafikia 11

Gari aina ya Fuso lililopata ajali kwa kugongana na basi mkoani Dodoma likiwa katika eneo la ajali. Picha na Maktaba.

Muktasari:

  • Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Dk Ernest Ibenzi, amesema majeruhi wawili wamepoteza maisha wakipatiwa matibabu.

Dodoma. Majeruhi wawili kati ya 11 waliokuwa wakipatiwa matibabu baada ya ajali ya basi la abiria na lori iliyotokea Chemba, mkoani Dodoma, wamefariki dunia, hivyo kufanya idadi ya vifo kufikia 11.

Ajali hiyo ilitokea alfajili ya jana, Alhamisi Septemba 18, 2025, na kusababisha vifo vya watu tisa, watano wanaume na wanne wanawake.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Dk Ernest Ibenzi, amesema majeruhi wawili wamepoteza maisha wakati wakipatiwa matibabu.

"Jana tulipokea majeruhi tisa, baadaye waliletwa wengine wawili waliokuwa wamefanyiwa upasuaji katika Hospitali ya Wilaya ya Chemba, kwa bahati mbaya hawa ndio walipoteza maisha," amesema.

Miongoni mwa waliofikishwa hospitalini, amesema ni mtoto mdogo wa umri wa chini ya mwaka mmoja ambaye ndugu wameshamtambua na kumtaja mama yake kuwa ni miongoni mwa majeruhi tisa waliofikishwa hospitalini akiwa hajitambui.

Awali, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa Umma wa hospitali hiyo, Renatha Mzanje, amesema miongoni mwa waliofariki ni mwanamke anayekadiriwa kuwa na miaka 35.

‎Kuhusu mtoto, Mzanje amesema: "Wakati anapata ajali alikuwa na mama yake mzazi ambaye amelazwa hapa, lakini bado hali yake siyo nzuri. Ndugu wameshafika na wamemtambua. Kwa sasa anaendelea na matibabu."

Akitoa taarifa kuhusu ajali hiyo jana, Septemba 18, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gallus Hyera, alisema chanzo ni uzembe wa dereva wa lori aliyehama upande wake wa kushoto na kwenda kulia, hali iliyosababisha magari hayo kugongana uso kwa uso.