Infinix yazindua Note 8 kwa watu wenye matumizi makubwa ya simu

Thursday November 26 2020
New Content Item (1)
By Mwandishi Wetu

Toleo jipya la simu ya Infinix 8 Note iliyozinduliwa hivi karibuni imebeba sifa kuu mbili za wepesi na nguvu zaidi. Ikiwa ni chapa ya simu janja inayofanya vizuri mtandaoni, Infinix kwa mara nyingine imevunja rekodi yake yenyewe kwa kuja na simu janja yenye kufanya kazi kwa ufanisi katika maeneo mengi ikikusudia zaidi soko la bidhaa la kati na hata la juu. Simu hii aina ya Infinix Note 8 inavutia machoni na inahamasisha wengine kuwa nayo.

Muundo huu uliokuja na simu hii ambao umebeba ndani yake MediaTek Helio G80 processor yenye uwezo mzuri wa kufanya kazi, kamera kubwa ya mbele na nyuma, kamera ya 64M Ultra HD 6, betri lenye Miliampia 64M Ultra HD 6, inajichaji kwa haraka na lenye kuhimili kukaa muda mrefu.

Ufanyaji kazi mzuri wa kila nyanja

MediaTek Helio G80 processor ikichagizwa na MediaTek HyperEngine Game Technology ambayo inaipa nguvu simu hiyo na kuiwezesha kufanya kazi kwa haraka na kuhakikisha kuwa simu hiyo inagusa maeneo mengine yote ya kimsingi kwa ufanisi. Chipset yenye sifa ya kufanya kazi vizuri imefungwa katika simu hiyo si tu kuifanya iwe nyepesi wakati wa matumizi bali inaifanya kuwa imara zaidi, pia inarahisisha kupata matokeo na taarifa za michezo mbalimbali.

MediaTek HyperEngine Game Technology inakufanya wakati wote ubaki na simu hiyo. Ni injini ya usimamizi makini wa rasilimali ambayo inahakikisha utendaji kazi mzuri wa muda mrefu na muda wa kutosha wa kucheza games mbalimbali, usimamizi wa CPU, GPU na memory kulingana na vipimo halisi vya umeme, masuala ya joto na games.

Inarahisisha games zinazochukua muda mrefu kufunguka kwa haraka na kucheza kwa ufanisi, zinatumika katika maeneo maalum na games zenye ukubwa. Simu hii imeongezewa ufanisi wa hali ya juu na maboresho ya uunganishwaji kwa minajili ya kuwezesha mtu kucheza game bila bughudha.

Advertisement

Malengo ni kuona mtumiaji wa Infinix Note 8 ambayo hukaa na chaji kwa muda mrefu na hujaa chaji kwa haraka. Betri hii inapewa nguvu na teknolojia ya hali ya juu (power marathon) iliyomo ndani ya simu janja ambayo hata kama chaji inakwisha inaiwezesha kutunza chaji kwa muda fulani. Kwa wale wanaopenda games, hii itawahakikishia wanakuwa na muda mrefu wa kucheza au kutazama. Kwa mfanyabiashara au mjasiriamali aliyefanikiwa, Note 8 inakupa uhakika wa uunganishwaji wakati unapotaka kuanza kuitumia, hali hiyo inakurahisishia kufanya mambo kadhaa ya msingi kama vile kutuma barua pepe, kutumia apps zinazohusu shughuli za kiofisi, kutumia apps za kufanya mikutano kupitia video na mengine zaidi.

Kukabiliana na simu kupata joto wakati wa kuchaji, Note 8 ina teknolojia ya injini mbili. Jambo hili linaifanya Note 8 kuwa ya baridi, ikipunguza joto kwa jotoridi 8 wakati inachajiwa.

Inaupeleka uzoefu mpya wa macho yako katika hadhi ya juu

Moja ya sifa kubwa zinazoitofautisha simu hii na simu nyingine ni kuwa na kamera kubwa mbili. Kioo chake kikiwa na uwiano wa 20.5:9 ambacho kina kamera ndogo mbili ambapo inakiwezesha kioo cha simu hiyo kuzunguka kufikia eneo la kamera kiasi cha kutoleta usumbufu ukiitumia kucheza wimbo, au kuangalia video kwenye simu.

Simu hiyo yenye kioo chake cha kisasa (6.95" Dual Infinity-O Display) kinasaidia kamera kuchukua picha zenye ubora kwa kuhakikisha hakuna vizuizi vyovyote vitakavyoharibu ubora wa picha.

Katika kuona namna bora ya kumpa uzoefu wa kipekee wa sauti na picha mtumiaji wa Note 8, simu hiyo imekuja na spika mbili zinazozunguka sauti ikiwamo DTS pamoja na njia zingine 4 ambazo zinakupa uzoefu wa aina yake wa kimuziki kwa ajili ya kukonga masikio na roho yako. Simu hiyo inampa fursa mtumiaji kuongeza kiwango cha sound effect ili kuweza kufurahia uzoefu wa sauti wakati wanaangalia filamu wanazozipenda au wanaposikiliza muziki au kucheza games.

Kurahisisha uchezaji wa video

Ili kuweza kukidhi mahitaji ya watumiaji wa simu janja katika kizazi cha 5 Mtandao wa Simu (5G), Infinix imefanya jitihada endelevu kadhaa kuboresha kazi za kamera za simu janja zake. Simu hii mpya aina ya Note 8 imekuja ikiwa tayari imewekwa kamera zenye ubora wa hali ya juu (64MP Ultra HD 6 Cameras) ambazo zitawawezesha watumiaji kuchukua matukio yote muhimu katika maisha katika namna ya kipekee, huku ikishajiishwa na ung’avu wa picha na kuakisi uzuri halisi wa yule aliyepigwa picha.

Katika dunia ya leo ya mitandao kama vile TikTok na vlogging, kuna uhitaji mkubwa wa kuzalisha video bora wakati wa matumizi ya simu. Baada ya kufanyiwa majaribio ya nguvu na tathmini ya kina na Timu ya Maendeleo ya Infinix, Program tumishi ya uboreshaji wa video ya Vidhance ilichaguliwa kwa kuwa ilikuwa ikizalisha video zenye ubora mkubwa. Hili lilitekelezwa rasmi kuanzia katika toleo la Note 7. Kwa sababu kampuni ya Infinix huwa haina mjadala linapokuja suala la utendaji kazi wa video na utulivu, Note 8 itakuwa na mfumo thabiti wa uboreshaji video (video-enhancement algorithms) unaoongoza sokoni kutoka katika Program tumishi ya Vidhance. Mfumo huu utahakikisha utulivu na ung’avu wa video wakati unapotumia Note 8. Tembelea  https://weareimint.com/.

Watumiaji wa simu hiyo wanabaki na chaguo la kucheza video hizo zikiwa katika mwendo wa taratibu, na kwa kuwa simu hiyo imeundwa ikiwa na sifa hizo bainifu, itaweza kuchukua kila tukio bila ya kuacha hata kitu kimoja.

Infinix pia imepata suluhisho la kukabiliana na mazingira ya mwanga mdogo ambalo limekuwa likiwasumbua watumiaji wakati wakichukua video. Kwa kutumia zaidi ya siku 180 (usiku na mchana) kufanya utafiti na maboresho kukabiliana na suala hili, simu hii ina mfumo maalumu wa kuiwezesha simu kufanya kazi katika mazingira ya giza (Note 8’s Ultra Night Mode 2.0) inakupa matokeo mazuri katika mazingira yenye mwanga hafifu.

Imebuniwa kwa ajili ya mafanikio

Muonekano wake utaweza kuwavutia watu mbalimbali na kwa namna simu hii ilivyo umuhimu wake utaongezeka maradufu kama ambavyo ilivyo muhimu kwa mtu kuvaa nguo mwilini mwake. Simu hii ina muundo mwepesi sambamba na GEM CUT ambayo imebuniwa kwa kuangalia mitindo inavyokwenda na hadhi yake. Uumbaji wa simu hii ambao bado ni mfano wa kuigwa umebebwa na mistari ya kipekee na uhalisia wa teknolojia. Muundo wake wa Gem Cut ni mahsusi kwa ajili ya muonekano wake na kudumu kwake. Utulivu katika simu hii ni mkubwa, kwa kuwa simu hii ya Note 8 ni imetengenezwa kuwawezesha watu kuishika bila woga wa kuiangusha.

“Tumejidhatiti kuzalisha bidhaa za kisasa zaidi ambazo ndizo zitakazokuwa mfano na kipimo cha sekta, hivyo tunajivunia kuzindua simu hii ya Note 8 katika masoko ya dunia. Bidhaa yetu ya kimkakati ya simu janja aina ya Note 8 imebuniwa na kutengenezwa kwa kuangalia changamoto za sasa na baadaye. Toleo hili jipya katika mfululizo wa simu zetu za Note, inaunganisha nguvu ya uvumbuzi wa kiteknolojia wa Infinix na mawazo yetu ya kina na kuyapeleka katika mahitaji halisi ya walaji ili kutoa uzoefu wa jumla ulioboreshwa katika muonekano, nguvu na ukaaji na chaji kwa muda mrefu. Simu ya Note 8 inafaa kwa watu wenye matumizi makubwa ya simu ambao wamezoea kuitumia kwa burudani mbalimbali na kwa kweli inatimiza matakwa yao yote,” anasema Aisha Karupa ambaye ni Ofisa Mahusiano wa Infinix, Tanzania.

Kwa muonekano wake, nguvu na ukaaji wake na chaji, Infinix Note 8 inadhihirisha uwezo wa kampuni ya Infinix iliyo nao katika kushughulikia mahitaji ya walaji pamoja na nguvu yake katika masuala ya kiufundi na uvumbuzi wa bidhaa. Simu hii aina ya Note 8 imetengenezwa kwa kuangalia simu za watu wenye matumizi makubwa zinaonekanaje, kwa sababu simu hii imesheheni muonekano na ubora kwa ajili ya kusaidia watu kuyaendea mafanikio katika maisha ambayo sisi sote tumekuwa tukiyatafuta.  Simu hii ni nyepesi zaidi, ina kasi zaidi na inakaa na chaji kwa muda mrefu zaidi, kiufupi hautakiwi kuikosa.

Upatikanaji

Note 8 inapatikana hapa nchini Tanzania kwa maelezo zaidi kuhusiana na Note 8, tafadhali, tembelea https://www.infinixmobility.com/tz/

Simu:+255 744 606 222Advertisement