Jafo achukizwa mwili wa mtumishi ulivyosafirishwa, aagiza mkurugenzi kusimamishwa kazi

Wednesday January 13 2021
New Content Item (1)
By

Dodoma. Waziri wa Tamisemi, Selemani Jafo ameagiza kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Tarime mkoani Mara, Jumanne Yassin kusimamishwa kazi kupisha uchunguzi baada ya halmashauri hiyo kusafirisha mwili wa aliyekuwa mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii,  Emanuel Joseph juu ya gari (kwenye carrier).

Emmanuel alifariki Januari 10, 2021 katika ajali ya gari iliyotokea mkoani Singida.

Leo jioni Jumatano Januari 13, 2021 katika mitandao ya kijamii  zilirushwa picha zikionyesha jeneza lenye mwili wa Joseph likiwa limefungwa juu ya sehemu hiyo ya gari.

Katika taarifa iliyotolewa leo na mkuu wa kitengo cha mawasiliano serikalini,  Nteghanjwa Hossea inaeleza kuwa Jafo amemuagiza katibu mkuu wa Tamisemi kuchukua hatua za kinidhamu kwa watumishi wote watakaobainika kuhusika na uzembe huo kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma.

Jafo amesema kitendo hicho ni kinyume na kanuni ya Q7(1-e) ya utumishi wa umma, mila na desturi za Watanzania.

Pia Jafo amewataka watumishi wa Tamisemi kujenga utamaduni wa kuheshimiana, kupendana na kuthaminiana wakati wote wanapotekeleza majukumu yao.

Advertisement