Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jela miaka 20 kwa kukutwa na kucha za mnyama huyu…

Mtwara. Mkazi wa Kijiji cha Miule wilayani Tandahimba, amehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 20 jela, baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na kucha ya mnyama ajulikanae kwa jina la Mhanga.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, ACP Nicodemus Katembo amesema, kesi hiyo ni kati ya kesi 76 zilizofikishwa katika mahakama mbalimbali na kutolewa hukumu.

“Yusuph Stephen Mkwemba (42) amekutwa na ukucha huo ambao ni nyara za Serikali nyumbani kwake, wenye thamani ya Sh1.52 milioni. Mahakama imemtia hatiani na kumfunga kwa kuwa ni kosa kisheria kuwa na nyara hiyo,” amesema.

Katika kesi nyingine, Mahakama ya Wilaya ya Masasi imemtia hatiani Yusuph Hamis Makuti (43) mkazi wa Mihima Masasi ambaye amehukumiwa kwenda jela miaka 30.

Mtuhumiwa huyo alikutwa na nyara za serikali (meno ya Tembo) vipande 24 vyenye uzito wa kilogram 43.8 sawa na tembo 6 wenye thamani ya Sh207.4 milioni.

Mtuhumiwa mwingine Abrahamu Bakari (41) mkazi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani ambaye amehukumiwa kwenda jela miaka 30 baada ya mahakama kumtia hatiani kwa kosa la kupatikana na bangi kilo 17.