Joe Biden na siku 100 za kuvaa barakoa nchini Marekani

Joe Biden na siku 100 za kuvaa barakoa nchini Marekani

Muktasari:

Rais mteule wa Marekani, Joe Biden amesema atawaomba raia wa nchi hiyo kuvaa barakoa kwa siku 100 za mwanzo za utawala wake ili kupunguza maambukizi ya virusi vya corona.

Dar es Salaam. Rais mteule wa Marekani, Joe Biden amesema atawaomba raia wa nchi hiyo kuvaa barakoa kwa siku 100 za mwanzo za utawala wake ili kupunguza maambukizi ya virusi vya corona.

 Biden  ameyazungumza hayo katika mahojiano na kituo cha televisheni cha CNN akibainisha kuwa ana amini kuwa jambo hili litasaidia kupunguza maambukizi ya virusi vya corona nchini humo.

Mbali na hilo, Biden pia amesema atatoa amri katika majengo yote ya serikali watu wavae barakoa.

"Siku ya kwanza nitakayoapishwa nitawaomba wananchi kuvaa barakoa kwa siku 100 na sio milele. Na nadhani itaweza kusaidia kupunguza maambukizi kwa kiasi kikubwa sana, kama chanjo na barakoa zitaweza kupunguza maambukizi,” amesema.

Marekani hadi sasa ina rekodi ya maambukizi ya corona milioni 14 na vifo 275,000.