Joto lawatesa wakazi Moshi

Muktasari:
Hali ya joto mjini hapa imeathiri mfumo wa maisha wa wananchi hasa uvaaji na ufanyaji kazi.
Moshi. Hali ya joto mjini hapa imeathiri mfumo wa maisha wa wananchi hasa uvaaji na ufanyaji kazi.
Gadson Mdee ambaye ni dereva bodaboda mjini hapa alisema hali ya hewa imekuwa nzito hali inayosababisha uchovu wa mwili na kujisikia kulala wakati wote.
“Unaweza ukafika kazini asubuhi na mapema na kuanza shuhuli zako, ikifika mchana mwili unakuwa mzito, uchovu na kupata usingizi,”alisema.
“Badala ya kufunga kazi saa saa tatu au saa nne usiku, unawahi kwa sababu ya hali ya hewa ilivyo nzito na mwili kuwa mchovu.”
Sophia Msofe, mkazi wa Mabogini alisema joto limeathiri uvaaji kwa kuwa analazimika kulala na nguo nyepesi.
“Siku hizi kulala na nguo ni kujitesa, joto ni kali,” alisema.
Yusufu Ramadhani ambaye ni mfanyabiashara mjini hapa alisema wakazi wa moshi wamezoea hali ya ubaridi.
(Maryasumta Eusebi)
“ Watu wa Moshi Tumezoea hali flani ya ubaridi ndio maana hali ya hewa iliyopo sasa hivi tunaona kama inatutesa, sehemu nyingine hali ya hewa ya joto hivi imezoeleka” Anasema Ramadhani
Anaongeza kuwa hata uuzaji wa maji baridi katika duka lake umeongezeka kutokana na wananchi wengine kupendelea kutumia maji baridi ili kukata kiu zao hasa majira ya mchana.
“Hapo nyuma nlikua nauza maji madogo ya kilimanjaro m katoni moja lakini sasa mpaka siku inaisha naweza kuuza katoni mbili au tatu”