JPM ateua kamishna wa TIRA na M/kiti bodi ya NHC

Dar es Salaam. Rais John Magufuli, leo (Jumamosi) amemteua Dk Baghayo Abdallah Saqware kuwa Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA).

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Dk Saqware ambaye anachukuwa nafasi ya Israel Kamuzora ambaye amestaafu, unaanza mara moja.

Kabla ya uteuzi huo Dk Saqware alikuwa Mhadhiri wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).

Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Blandina Nyoni kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

Nyoni anachukua nafasi iliyoachwa wazi na  Zakia Hamdan Meghji ambaye amemaliza muda wake.