Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

JPM mgeni rasmi siku ya mazingira duniani

Muktasari:

  • Maadhimisho hayo yatafanyika jijini Dar es Salaam

Mkuu wa wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva amesema Rais John Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya mazingira duniani yanayofanyika kila Juni 5 kila mwaka.

Kuelekea siku hiyo, Lyaniva amesema maadhimisho hayo yatafanyika jijini humo, huku akiwataka maofisa mazingira wa wilaya hiyo kuhakikisha wanatumia sheria ya utunzaji wa mazingira, kukabiliana na watu wanaotupa taka hovyo.

Pia, amewakata maofisa hao kuondoa marundo ya takataka zilizorundikwa pembezoni mwa barabara zote za manispaa hiyo, kwani kwa kufanya hivyo itasaidia kutunza mazingira na kuweka wilaya hiyo katika hali ya usafi na kuepuka mlipuko wa magonjwa.

Lyaniva alisema hayo leo Jumatano Mei 30, 2018 wakati wa ufunguzi wa wiki ya mazingira duniani ambapo pamoja na mambo mengine, manispaa hiyo imepanda miti na kufanya usafi katika wodi ya wagonjwa wa Kipindupindu iliyopo katika hospitali ya Rufaa ya Temeke.

“Nataka  Sheria ya mazingira itumike katika kutunza mazingira yetu, sitaki kuona marundo ya takataka katika barabara zilizopo ndani ya Manispaa yangu, wahakikishe kuwa wao wanakuwa wa kwanza kusisitiza wananchi wanaondoa takataka zote zilizopo ndani na nje ya hifadhi ya barabara ikiwemo matairi ya magari,” amesema Lyaniva.

 “Kwa wale ambao ni wakaidi au wana mioyo migumu, sheria ichukue mkondo wake, sisi hatutavumilia tutachukua hatua kali dhidi ya yoyote atakayebainika kufanya uharibifu wa mazingira bila kujali wadhifa wa mtu.”

Lyavina alisema maadhimisho ya siku ya mazingira kitaifa, yatafanyika jijini hapa na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais John Magufuli.

Awali, Ofisa Mazingira kutoka Manispaa ya Temeke, Castory Alexanda alisema Juni 5 ya kila mwaka, dunia huadhimisha siku ya mazingra na kwamba kwa hapa nchini, kauli mbiu ya maadhimsiho hayo ni 'zuia uharibifu wa mazingira unaotokana na taka za plastik'.

“Ili kutekeleza jitihada ya kupunguza matumizi ya nishati itokanayo na miti mkoa wa Dar es Salaam, tumegawa majiko 4500 kwa wajasiriamali, lengo likiwa ni kutumia nishati mbadala kwa ustawi wa mazingira na maliasili,” alisema Alexanda.