Kabendera akiri makosa

Muktasari:

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemhukumu mwandishi wa habari, Erick Kabendera kulipa fidia ya Sh172 milioni baada ya kukutwa na hatia ya kukwepa kodi.Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemhukumu mwandishi wa habari, Erick Kabendera kulipa fidia ya Sh172 milioni baada ya kukutwa na hatia ya kukwepa kodi.

Pia Mahakamani hiyo imempiga faini ya Sh250,000 kwa kosa hilo la kukwepa kodi.

Katika shtaka la kutakatisha fedha, mahakama imemhukumu Kabendera kulipa faini ya Sh 100 milioni na tayari ameshailipa.

Hukumu hiyo imetolewa leo Jumatatu Februari 24, 2020 na Hakimu Mkazi Mkuu, Janeth Mtega  baada ya mshtakiwa kukiri mashtaka yake kwa njia ya majadiliano na Mwendesha Mashtaka wa Serikali ya Tanzania (DPP).