Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kada wa CCM anayedaiwa kumwagiwa tindikali atoa neno

Idrissa Makishe, mmoja wa makanda wa Chama cha Mapinduzi(CCM) ambaye anadaiwa kumwagiwa tindikali.

Muktasari:

  • Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amesema bado wanaendelea na uchunguzi, wahusika watakapobainika watafikishwa mahakamani

Moshi. Wakati Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro likisema linaendelea na uchunguzi wa tukio la kada wa Chama cha Mapinduzi(CCM), Idrissa Makishe (38) anayedaiwa kumwagiwa tindikali, amesema angepata huduma ya kwanza haraka asingepata madhara makubwa.

Makishe ambaye amelazwa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini, KCMC amesema baada ya kupata shambulio hilo, alikimbia kuomba msaada kwa wananchi, lakini walikuwa wakimkimbia badala ya kumsaidia.

Kada huyo ambaye ni mkazi wa Njoro Manispaa ya Moshi na dereva bodaboda, alipatwa na madhila hayo usiku wa Septemba 20, mwaka huu baada ya mtu mmoja kumkodi akitaka ampeleke eneo la Njoro lililopo wilayani hapa.

Alipoulizwa na Mwananchi Digital kama kuna watu wamekamatwa au kuhojiwa kuhusiana na tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amesema bado wanaendelea na uchunguzi, wahusika watakapobainika watafikishwa mahakamani.

"Uchunguzi unaendelea ukikamilika watakaokuwa wamepatikana tutakapowapeleka mahakamani, tutawajulisha,"amesema Kamanda Maigwa.

Akizungumza akiwa hospitali hapo, Makishe amesema anamshukuru Mungu anaendelea vizuri licha ya kwamba uwezo wake wa kuona umekuwa mdogo kwa kuwa jicho moja halioni kabisa na moja linaona kwa mbali.

Makishe ambaye alipata majeraha sehemu mbalimbali ikiwamo usoni na mikononi, amesema siku ya tukio alipokimbia kuomba msaada watu walimkimbia badala ya kumsaidia.

"Namshukuru Mungu naendelea na matibabu vizuri, jicho moja la kushoto ndilo limeanza kuona kidogo lakini jicho la kulia halioni kabisa, hivyo uwezo wangu wa kuona ni mdogo bado sijaweza kuona kitu kwa uhalisia wake,"amesema.

"Jicho la kulia sioni, naendelea na dawa na baada ya muda madaktari ndio watakuja kuniambia nini cha kufanya kiutaalamu zaidi maana lenyewe ndilo limeathirika zaidi."

Ametoa wito kwa Watanzania kujenga utamaduni wa kusaidia wenzao wanapopata matatizo na kupiga kelele za kuomba msaada, akieleza kuwa siku ya tukio alipopiga kelele watu walimkimbia badala ya kumsaidia.

 "Watu walikuwa wananikimbia, maana jicho moja lilikuwa linaona kwa mbali lakini niliona watu wakinikimbia wakati napiga kelele kuomba msaada, naziomba mamlaka husika zitoe elimu kwa Watanzania juu ya matukio kama haya ili wafahamu namna ya kutoa msaada, waelimishwe wakiona mtu anapata shida wajitokeze kutoa msaada," amesema Makishe.