Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kamati ya Bunge yapigwa butwaa ‘Viagra’ inavyotumika tofauti

Dawa zilizokamatwa na mamlaka ambazo hazijasajiliwa wengi wakifahamu kama Viagra

Muktasari:

  • Kamati ya kudumu ya Bunge ya Afya na masuala ya Ukimwi yatembelea Mamlaka ya Dawa na Vifaatiba waonyeshwa dawa bandia na kuelezewa matumizi mabaya ya viagra.

Dar es Salaam. Mamlaka ya Dawa na Vifaatiba imekamata dawa aina ya Sildenafil Citrate 'Viagra' kwa kutosajiliwa na wengine wakitumia tofauti na maelekezo.

 Hayo yamesemwa leo Septemba 11, 2923 jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Adam Fimbo alipokuwa anawaelezea Kamati ya Bunge ya Afya na masuala ya Ukimwi walipotembelea ofisi hizo.

Amesema kuna baadhi ya watu wanatumia viagra kwa ajili ya kuongeza nguvu za kiume wakati matumizi halisi ya dawa hizo ni kutumika kwa kupitia maelekezo ya wataalamu wa afya.

Fimbo nasema kitu cha kwanza unapopata tatizo lazima kumuona daktari ili akupe maelekezo lakini wengi wao wanatumia vidonge hivyo bila kufuata maelekezo ya daktari kwa ajili ya kumkomoa mwanamke.

"Viagra haitakiwi kutumika kwa mtu mwenye presha kwa kuwa inaenda kuongeza presha na kusababisha kupasuka kwa mishipa ya fahamu na hata kupelekea mtu kupooza mwili wengine kufariki," amesema Fimbo.

Amesema hawana takwimu sahihi za watu wangapi wamefariki kutokana na matumizi ya viagra lakini inatakiwa kuzingatiwa matumizi sahihi ya dawa hizo.

Hata hivyo Fimbo amewataka wagonjwa kutoa taarifa za madhara wanayoyapata kutokana na matumizi ya dawa wanazotumia ili kufanyiwa uchunguzi wa haraka.

Pia Fimbo amesema wamekamata baadhi ya dawa bandia ambazo hazina kiambata hai,dawa zililizochini ya kiwango na zisizosajiliwa na mamlaka.

"Ili kufanyia uchunguzi wa dawa husika tunapokea taarifa kutoka kwa wagonjwa kutokana na madhara walioyapata inawezekana ikawa ni madhara ya ugonjwa au matumizi ya dawa hivyo tunafanyia kazi kwa haraka kwa kupeleka sampuli za dawa husika katika maabara," amesema Fimbo.

Amesema katika ukaguzi wamekutana na dawa ambazo hazijasajiliwa ikiwepo Viagra ambazo zinatumika isivyosahihi.

Pia amesema wameshapeleka baadhi ya kesi mahakamani zipo walizoshinda na nyingine kushindwa kutokana na ushahidi kutojitosheleza na pia zipo kesi zilizoliopiwa faini.

Fimbo amesema kumekuwa na tabia ya baadhi ya watumishi wasikuwa na maadili ya kutoa dawa kwa siri na kuzipeleka nje ya sehemu elekezi za kupatikana kwa baadhi ya dawa.

"Kuna baadhi ya dawa hazitakiwi kuuzwa nje ya hospitali za serikali lakini unaenda kuzikuta katika maduka ya dawa ya nje huku baadhi ya dawa zikiwa zimefichwa nembo,"amesema.

Pia Fimbo amesema kumekuwa na tabia ya watu kubadilisha dawa za kwenye makopo kwa kuweka jina la dawa ambazo haziendani na jina la dawa.

Baadhi ya dawa bandia zilizokamatwa ni Sonaderm, Gentrisone na Zenoxyl huku zilizochini ya kiwango ni U-Sol, Spamox ambazo huota ukungu (Fangasi) na unga wa dawa kuganda.

Pia zipo dawa ambazo zina maandishi ya serikali lakini imewekwa nembo ya MSD ambazo ni Benzathine, Hydralazine, Ampimax huku Lumerax na Combiart  zimeandikwa haziuzwi (For gov-tz not for sale)

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya Ukimwi, Stanslaus Nyongo alitaka kufahamu ni namna gani wanafikisha taarifa kwa wananchi na namna wanavyopata mrejesho.

"Ili kusaidia madhara yasiendele na wale walioleta taarifa wanapewa vipi majibu yao kutokana na kile walichokieleza?” aliuliza Nyongo.

Fimbo amesema wamejaribu kutumia waandishi wa habari na kupeleka matangazo baadhi ya vituo vya runinga lakini changamoto kubwa inayokuja ni gharama za kutoa matangazo husika.

Akielezea changamoto wanazokutana zao katika kupokea ujumbe wa msaada wa madhara ya dawa ni kukutana na ujumbe usiohusiana na jambo husika ikiwepo kuomba mikopo na kupewa salamu.