Kanisa lawaita wananchi wakahamishe makaburi ya wapendwa wao

Muktasari:

  • Wakazi wa Vwawa wilayani Mbozi Mkoa wa Songwe waliozika ndugu katika makaburi ya  Kanisa Katoliki  la Mtakatifu Patrick Parokia ya Vwawa  wametakiwa kufika  kanisani hapo kupata utaratibu  wa kuhamisha  makaburi.

Songwe. Wakazi wa Vwawa wilayani Mbozi Mkoa wa Songwe waliozika ndugu katika makaburi ya  Kanisa Katoliki  la Mtakatifu Patrick Parokia ya Vwawa  wametakiwa kufika  kanisani hapo kupata utaratibu  wa kuhamisha  makaburi.

Paroko wa Parokia hiyo, Padri  Dennis Hula amesema hayo alipozungumza na Mwananchi Digital  jana Desemba17, 2021 ofisini kwake kuwa wamepanga kuhamisha makaburi hayo kwa kuwa  wanahitaji  eneo hilo kwa matumizi mengine na ni  eneo la kanisa hilo.

"Tunaheshimu marehemu na tunajali utu kwa hiyo ndio sababu tumeamua kutangaza  kwamba kila ambaye anajua ameshawahi kuzika ndugu yake katika eneo hili aje atoe taarifa zilizokamili na ikipendeza aje na watu kadhaa waliyoshuhudia Ili taratibu ziweze kuchukuliwa na kanisa," amesema.

Mkazi wa Vwawa, Yusta Kayuni amesema itakuwa mara ya kwanza kwake tangu azaliwe kuona makaburi yanahamishwa licha ya kuwa ana ndugu zake watatu waliozikwa hapo.

"Najiuliza sana siku itakapofika siku  ya kuyaondoa masalia ya ndugu zangu itakuwaje sipati majibu," amesema