Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Katikakatika umeme, Kongani la Viwanda Kilimanjaro kufungiwa transfoma yake

Mmoja wa wafanyakazi akitoa maelezo kwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga ya namna ya kuendesha mtambo wa kutengeneza mabati katika kiwanda cha mavati kilichopo ndani ya  kongani la Viwanda Kilimanjaro,Wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Muktasari:

  • Kongani hilo linalotarajiwa kuwa na viwanda 20,litakapomalizika litaweza ku,alisha ajira zaidi ya 30,000

Dar es Salaam. Kongani la Viwanda la Kilimanjaro lililopo Mwasonga Wilaya ya Kigamboni Jijini Dar es Salaam, linatarajiwa kufungiwa transifoma yake ili kukabiliana na adha ya kukatika mara kwa mara kwa umeme.

Ahadi hiyo imetolewa na Waziri wa Viwanda na biashara,Judith Kapinga, alipotembelea kongani hilo  kuangalia hali ya uzalishaji na kusikiliza changamoto wanazokabiliana nazo.

Kapinga amesema katika ziara hiyo moja ya changamoto alizopokea  ni upakanaji wa uhakika wa umeme hali wanayohifia kuathiri uzalishaji.

"Nimeambiwa hapa kuna changamoto ya upatikanaji wa umeme licha ya Tanesco kuwahi kuwafungia laini yao,hivyo nimeshawasiliana na Waziri wa Nishati na Tanesco ya hapa Kigamboni kwamba wafungiwe transfoma yao ili kuondoa adha hii,"amesema.

Ukiacha umeme pia wazalishaji hawa wametaka uwepo wa matumizi ya gesi ambayo mbali na kusaidia uchakataji wa bidhaa lakini pia itasaidua kupunguza gharama za uendeshaji.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga akizungumza na waandishi wa habari katika ziara aliyoifanya kwenye kongani la Viwanda la Kilimanjaro lililopo Mwasonga Wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam

Katika kulishughulikia hilo,Waziri Kapinga amesema tayari amewasiliana na Shirika la Maendeleo la Mafuta na Gesi(TPDC),kuona namna watakavyoweza kufikisha miundombinu ya nishati hiyo maeneo hayo.

Akizungumzia hali ya uzalishaji alivyoiona, Kapinga amesema moja ya mambo yaliyomvutia ni kuongeza thamani ya bidhaa ikiwemo kuchakata chupa wenyewe katika uzalishaji wa kiwanda cha vinywaji laini na kwa kutumia malighafi za hapa nchini.

Jingine amesema ni kuona vijana wadogo waliopewa ajira na ujuzi ambao awali hawakuwa nao na hivyo kuisadia serikali katika kuzalisha ajira kwa vijana kwani katika viwanda  viwili vilivyoanza uzalishaji tayari ajira 5000 zimezalishwa.

Akizungumza kwa niaba ya uongozi wa Wakurugenzi , Aisha Mohammed, amesema kongani hili lipo chini ya kampuni za GSM na lina  karibu heka 300 ambazo zitatumika kujenga viwanda 20.

Aisha amesema lengo la kongani hili ni kuleta viwanda pamoja na kurahisiha uzalishaji lakini pia kutimiza ndoto za serikali kuwa na viwanda vingi ambayo ni moja ya malengo yaliyopo katika dira ya 2050.

"Pamoja na yote haya nitumie nafasi hii kushukuru namna ambavyo serikali imekuwa wepesi kututatulia changamoto za kimiundombinu tunazokumbana nazo  ikiwemo barabara ya Mwasonga ambayo baada ya kujengwa  imerahisisha katika suala zima la usafirishaji malighafi na bidhaa baada ya kuzalishwa.

Hata hivyo Aisha amesema wakati mpaka sasa ni viwanda viwili vimeshajengwa kwenye kongani hilo ambapo ukiacha cha vinywaji laini kipo kiwanda cha mabati ambapo baada ya kumalizika kwa viwanda vingine 18 ajira zaidi ya 30,000 za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja zinatarajiwa kuzalishwa.

Aisha Mohammed,mmoja wa wakurugenzi wa kampuni za GSM, akizungumza katika ziara ya Waziri wa Biashara na Viwanda, Judith kapinga alipotembelea kongani za viwanda vya Kilimanjaro

Naye Mhandisi na Meneja Uzalishaji  wa kiwanda cha mabati, Abdullatif Said, amesema lengo lao ni kufanya uzalishaji wa bidhaa zilizo bora na sanifu  zaidi lakini wakati huohuo kupunguza uchafuzi wa mazingira.

Kwa upande wake Elia Dambani, mmoja wa wafanyakazi katika viwanda hivyo ameishukuru serikali kwa namna inavyoshirikiana na wawekezaji kwani imechangia vijana na wao kupata ajira.

Katika wito wake, Dambani ameomba hali hiyo ya kuchochea kuongeza viwanda iendelee kwani itawezesha kupunguza vijana wakabaji mtaani na kusaidia kuinua uchumi wa mtu mmojammoja na Taifa kwa ujumla.