Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kauli mbili za mwisho za Hayati Mrema hizi hapa

Kauli mbili za mwisho za Hayati Mrema hizi hapa

Muktasari:

  • Miongoni mwa kauli zake ni pamoja na kutaka kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi, huku akishauri mchakato wa kupatikana kwa Katiba mpya uendelezwe pale ulipoishia.  

Dodoma. Ni mwisho wa enzi, ndivyo unavyoweza kueleza kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha TLP, Augustino Mrema ambaye kabla ya kifo chake alisisitiza umuhimu wa kupatikana kwa Tume huru ya uchaguzi ili isimamie chaguzi zote kwa msingi wa haki.

Alitoa kauli hiyo Julai 14, 2022 baada ya kuwasilisha maoni yake mbele ya Kikosi Kazi cha kuratibu maoni ya wadau wa demokrasia ya Vyama vingi vya siasa, huku akibainisha kuwa tume huru itarejesha uaminifu kwa wagombea.

“Tunahitaji tume huru na hii ni muhimu sana. Kuwe na chombo huru cha kusimamia chaguzi kwa nafasi zote zinazojitokeza ikiwemo kwenye Serikali za Mitaa, vijiji na serikali za vitongoji.

“Tume ni kitu muhimu sana katika kusimamia haki na baadae tuje na Katiba,” alisema.

Kuhusu Katiba mpya Hayati Mrema alishauri mchakato ulioanza uendelezwe hadi ufikie mwisho huku akitahadharisha kutokuanza upya akihofia gharama kuwa kubwa zinazoweza kutumika.

Kauli nyingine aliyotoa Julai 14 Dar es Salaam kutambulisha rasmi mke wake wa ndoa Doreen Kimbi kwa watanzania  huku akiwaeleza waandishi kumpatia mke wake wadhifa wa waziri wake wa ulinzi.

Kuhusu kumtambulisha mke wake Mrema alisema Doreen alifunga naye ndoa kwa shabaha ya kumtunza na kumsaidia kwenye shughuli zake za kisiasa.

"Toka nimefunga ndoa yangu sijawai kuja Dar es Salaam kumtambulisha mke wangu mbele ya vyombo vya habari. Mnataka nimtambulishe?” aliwahoji waandishi wa habari.

Akaendelea, “Anaitwa Doreen Kimbi ni mke wangu na ni Waziri wangu wa Ulinzi ananisaidia shughuli zangu za kisiasa."

Katika kuhitimisha mazungumzo yake ambayo hayakuzidi dakika saba, katika ofisi ndogo za Bunge, aliwataka Watanzania kuendelea kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan ili aweze kukamilisha ndoto yake ya kujenga mifumo imara ya kuwatumikia na kuwaletea maendeleo Watanzania.