Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Samia amlilia Mrema

Rais Samia amlilia Mrema

Muktasari:

  • Mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania aliyewahi kuwa mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), NCCR-Mageuzi na TLP amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole kwa famialia ya Agustino Mrema na Chama cha TLP kufuatioa kifo cha mwanasiasa huyo mkongwe.

 Mrema (77) aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, amefariki dunia leo Jumapili, Agosti 21, 2022, asubuhi, katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam.

Msemaji wa MNH, Aminieli Eligaisha amesema, Mrema alilazwa hospitalini hapo kuanzia Agosti 16, 2022 na kufikwa na mauti asubuhi ya leo.

Muda mfupi baada ya taarifa za kifo cha Mwenyekiti huyo chama cha TLP, Rais Samia alituma salamu za rambirambi kwa familia na TLP.

“Nimesikitishwa na kifo cha Mwenyekiti wa chama cha TLP Bw. Agustino Lyatonga Mrema kilichotokea leo asubuhi Jijini Dar es Salaam.

Nitamkumbuka kwa mchango wake katika mageuzi ya siasa, uzalendo na upendo kwa Watanzania. Pole kwa familia na wana TLP. Mungu amweke mahali pema. Amina” ameandika Rais Samia kupitia ukurasa wake wa Twitter

Enzi za uhai wake, mwanasiasa huyo aliwahi kuwa mgombea urais kupitia NCCR-Mageuzi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 1995 baada ya kujiunga na chama hicho akitokea Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Aidha, Mrema aliwahi kuwa Mbunge wa Moshi Vijijini (CCM), Temeke (NCCR Mageuzi) na Vunjo kupitia TLP na hadi amefikwa na mauti alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Parole.